Pages

Friday, July 12, 2013

DIDA APIGWA DONGO


BAADA ya hivi karibuni Mtangazaji wa Radio Times, Khadija Shaibu ‘Dida’ kufunga ndoa na mwanaume aitwaye Ezden, mashosti zake wamemtaka kutulia sasa na asijaribu kugeuza ndoa kuwa fasheni. Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya mastaa walioomba hifadhi ya majina yao ambao walihudhuria ndoa hiyo iliyofungwa Ijumaa iliyopita Ubungo jijini Dar walisema, wamechoka na mialiko ya ndoa zake kila baada ya kipindi kifupi hivyo ni wakati sasa wa kutulia, Hii ni ndoa ya Tatu ya Dida.

“Asifanye ndoa kama fasheni, tumechoka kuhudhuria sherehe za ndoa yake, kama ana kasoro, ajirekebishe ili atulie sasa ajenge maisha yake,” alisema staa mmoja ambaye ni rafiki wa karibu na ndugu wa Dida. Hata hivyo, akizungumzia kuhusu kuolewa huko, Dida alisema safari hii ndoa yake ikivunjika haolewi tena.


WAKENYA WAMKOSOA PREZZO




Msanni Prezzo wa Kenya  atakuwa amepata sample ya majibu ya baadhi ya fans wake ambao wengi ni wakenya baada ya kumdiss Diamond Platinumz wa Tanzania kupitia akaunti yake ya twitter July 10.


Sample ya majibu hayo inaweza kuonekana kupitia comments zote za fans kwenye habari iliyowekwa na mtandao wa ghafla wa nchini Kenya, ambapo asilimia 99 wameonesha kutokubaliana na alichokifanya.



Edwin Mwashegwa  : ah, Diamond achana na huyu mbulula, wewe unda hela!, bifu za kisenge hazifai.



Top Commenter: Prezzo umepita hiyo age ya beef za kishenzi. Ingia studio utoe kitu, otherwise kwa musiki diamond ako juu. I feel you bro! anything to remain relevant and grab some headlines.



Bellah Ongachi : aaarggh Diamond is waaayy better.. n am sure by the time he hits the years prezzo has stayed in the entertainment scene he'll be miles ahead..so your thing diamond.



Caroline Karijo : Mhhhhh who even listens to to him Jaguar and Diamond r much better than him n we all knw,,,,,,, he can continue playing women who stoops low for him.



Yvonne De Cole : Prezzo ni wivu nini,,,, leave the highest paid musician in East Africa alone,,, ana mulla en he is still simple doesn floss,,,, prezzo inherits yet flosses



De Sheriff : Diamond, silence is the best weapon. let the baby throw tantrums. Prezzo, its tym to mature up.



Diamond hadi sasa bado hajazungumza chochote.

TUTAKUCHAKAZA WEWE KAGAME NA RWANDA YOTE



SERIKALI ya Tanzania imeipa onyo kali nchi ya Rwanda ikiitaka isijaribu kuota ndoto za kuishambulia kijeshi, vinginevyo itajibu mapigo kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa imeichakaza.


Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania.


Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame.


Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana.


Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, Kagame anadaiwa kusikika akitoa matamshi ya vitisho dhidi ya Rais Kikwete, kwamba anamsubiri katika wakati aujuao na kumchapa.


Baadhi ya maneno yanayodaiwa Rais Kagame aliwaambia vijana waliokutana katika mkutano wao uliojulikana kama ‘Youth Konnect’ na kufadhiliwa na mke wake, Janet Kagame, yanasema: “Huyu mtu mliyemsikia akiwa upande wa Interahamwe na FDLR na akashauri majadiliano….majadiliano?”


Aidha, Kagame anadaiwa kusema kuwa hatakuwa tayari kujadili jambo hilo, isipokuwa atamsubiri Rais Kikwete sehemu muafaka na ‘kumtandika’.

“Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani,” alikaririwa akisema Rais Kagame, akilenga kumtisha Rais Kikwete.


Mbali na Kagame, baadhi ya viongozi kadhaa wa serikali ya Rwanda wamekuwa wakimshambulia Rais Kikwete wakimpachika majina ya kejeli ya; “Rais mhurumia magaidi, wauaji wa kimbari, mkorofi na mwenye dharau.”


Mkumbwa hata hivyo alisema Serikali ya Tanzania haina sababu ya kuingia katika vita na Rwanda, kwa sababu tu ya ushauri alioutoa Rais Kikwete wa kuitaka ikutane na wapinzani wake wanaoishi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kujadiliana kuhusu amani ya nchi za Maziwa Makuu.


Alisema msimamo wa Tanzania utabaki kuwa uleule wa kuitaka nchi hiyo ikubali kukaa meza moja na wapinzani wake, ili kumaliza migogoro inayoendelea katika nchi hizo za maziwa makuu, ambao unaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na SADC.

“Unajua mgogoro wa DRC na Rwanda hauwezi kumalizika bila ya nchi hizo kukaa meza moja na wapinzani wao ili kupata suluhu ya kudumu,” alisema Mkumbwa.


Aliwataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao kama kawaida, kwani serikali yao iko makini katika kulinda mipaka yake.

Chanzo cha mzozo
Msuguano baina ya nchi hizi mbili ulianza siku chache tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Rais Kikwete wakati akimtaarifu Rais Museveni kile walichokuwa wamekijadili katika kikao hicho kwa vile aliketi kwa muda kwa kuwa alichelewa kuwasili, alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zifungue mlango wa mazungumzo na waasi wao na akaanza kutaja majina ya vikundi vya uasi vya nchi hiyo vilivyopo nchini DRC.

Habari zinasema kauli ya Rais Kikwete iliungwa mkono na Rais Museveni akisema: “Bila mazungumzo hatutafika popote pale”.  


Hata hivyo, matamshi hayo yalijibiwa kwa ukali na serikali ya Rwanda, kiasi cha kumlazimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kutoa tamko bungeni.


Kwa kauli yake, Membe alisema serikali ilikuwa imeshangazwa na shutuma hizo za Rwanda kwani halikuwa jambo baya kutoa ushauri uliolenga kuleta mapatano na kuepusha umwagaji zaidi wa damu wa wananchi. 

Akaongeza kuwa, ilikuwa ni wajibu wa Serikali ya Rwanda kuupokea ama kuukataa, na wala si kutoa maneno ya kejeli na vitisho.

Kauli ya Zitto
Akizungumzia kauli hiyo ya vitisho, mwanasiasa machachari hapa nchini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, alisema ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda ulikuwa wa busara mno na akashangaa kuona nchi hiyo jirani ikitoa vitisho, kejeli, dharau na ukosefu wa adabu kwa Kikwete.
 
Katika moja ya tamshi lake alilolitoa jana katika mitandano ya kijamii, Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema Marekani wanaongea na waasi wa kundi la Taliban, hivyo hakuna dhambi kwa Rwanda pia kufanya hivyo.

“Pia kama hutaki ushauri si unakataa tu, sasa kuanza kurushiana maneno ya nini tena? Hutaki ushauri basi. 

Maneno ya kila siku ya nini? Tangu Kikwete amesema kule Addis, hajasema tena. Membe (waziri) akajibu Dodoma Tanzania haijasema tena. Kigali inasema mambo haya kila siku kwa ajili ya nini?


Taliban na Al Qaeda si wale wale? Wale watoto waliozaliwa mwaka 1994 na wakimbizi wa Kihutu waliopo Kongo nao ni wauaji? Tufikiri vizuri mambo haya. Kuna ‘genociders’ wasakwe, wakamatwe wahukumiwe. Kuna watu wana haki kabisa ya kutaka kushiriki kwenye siasa za Rwanda na wanazuiwa, wameshika silaha. Hawa lazima wakae meza moja wakubaliane,” alisema Zitto.

Mwanasiasa huyu alisema kwa sasa serikali za nchi hizo mbili zinatakiwa kuingia katika vita ya kupambana na kuondoa umasikini wa watu wake na si vita ya mtutu wa bunduki.

Busara itumike kwa viongozi ‘neutral’ kama Uhuru Kenyatta kuwaweka pamoja Kagame na Kikwete wamalize tofauti zao. Haya maneno hayana maana yoyote,” alisema.

Alisema vita haitamuumiza Rais Kagame wala Rais Kikwete na familia zao, bali itaumiza wananchi wa kawaida wa mikoa ya Kagera na Kigoma na mikoa ya mpakani ya Rwanda.


Vita itaturudisha nyuma sana kwenye juhudi za maendeleo. Vita itazima harakati za kujenga demokrasia nchini.  Busara itumike tu,” alisema Zitto.

Tanzania Daima

STRESS: Fahamu njia rahisi za kukabiliana na msongo wa mawazo

Florah Amon Nkondola (Binti Sayuni)
Msongo wa mawazo ama stress kwa kiingereza, ni tatizo ambalo kwa bahati mbaya sana limeendelea kuwa kitu cha kawaida sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo. Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili.
Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili. Hapa ni baadhi tu ya njia zilizo rahisi ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na hali hii pindi unapojikuta umetumbukia ndani yake
1. Jifunze kusema “hapana” hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako… sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.
2.Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, unajua ukikaa chini na kufikiria utagundua kuna mtu flani au kundi flani la watu ndo linalokuleta msongo wa mawazo, sasa kaa nao mbali kabisa.
3. Simamia mazingira yanayokuzunguka. Mazingira yanakuzunguka yanaweza kuwa sababu ya stress zinazokukumba, mazingira yapo nayozungumzia mimi hapa? njia unayotumia kwenda kazini au kurudi nyumbani ina foleni sana? hiyo nayo inawea kuwa sababu ya stress ulizonazo, lakufanya epuka matumizi ya barabara kwa wakati huo, mazingira ya soko wakati wakufanya manunuzi ya bidhaa mbali mbali yanakupa stress? nenda katika supermarket maana kwa kiasi flani kuna utulivu na hali ya hewa nzuri
4.Epuka Hasira za haraka, kuna ya mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka nao ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi
5.Tengeneza orodha ya vitu anavyotaka kufanya sikuhiyo asubuhi tu ukiamka, mara nyingi unapaswa kujua mambo ambayo ni ya lazima kuyafanya kwa siku ambayo unaianza ili ikifika jioni usiwe na viporo, katika orodha yako tenganisha orodha hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa mawazo.
Naomba niishie hapa kwa leo maana nimewaonjesha yale ninayoyajua na ambayo nimejifunza, swala la kuondoa msongo wa mawazo linapaswa kuangaliwa kiundani zaidi maana ni pana sana, hapa juu nimeongelea kuepuka stress ambazo si za muhimu ila kuna swala la saikolojia ambalo kwa kadiri siku zinaendelea, tutaligusia.
Unaweza kuungana na mwandishi wa makala hii kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa kubonyeza hapa