Abela akiwa anagonga nyundo.
Dada Abela
alizungumzia takribani mambo matano ya msingi, somo lilibeba kichwa
kisemacho '' JINSI YA KUJIENDELEZA KIFANI ''_ How can we develop our
carrier!
1. TAMBUA KUSUDI LAKO DUNIANI.
2. MAONO YAKO DUNIANI NI NINI
3. UNAPENDELEZ NINI (VALUES/INTERESTS)
4. UNA HAIBA YA AINA GANI (PERSONALITY)
5. ANGALIA FURSA ZAKO (EXPLORE YOUR POSSIBILITIES)
Hivyo ni vidokezo tu (highlights) ya vile alivyofundisha na alifafanua kwa kina sana.
Robert naye aliachilia nyundo zake!
Alizungumzia
mambo makuu ya msingi. Sitatoa maelezo bali nakupa dondoo tu ya kile
alichozungumza. Ukitaka ufaidi vizuri unakaribishwa NCHI YA AHADI, Sinza
Kamanyola; DSM
DONDOO/HIGHLIGHTS
1. KUJIAMINI
2. KUJIZUIA/KUWA NA NIDHAMU
3. UVUMILIVU.
Rose Tarimo alitoa ushuhuda wenye kujenga sana sio kusisimua!
Dada Rose
Tarimo ni moja kati ya watu ambao wanastahili kufuatwa as a role modal.
Huyu dada baada ya kumaliza elimu ya msingi alikaa nyumbani miaka nane
lakini ndani yake alikuwa na shauku kuu ya kutaka kusoma wakati huo hana
mtu wa kumsomesha!
Aliamua
kukusanya madaftari ya wanafunzi wa sekondari na kuanza kujisomea
mwenyewe bila ya mwalimu, baadae akanunua namba ya mtihani. Akafanya
mtihani akapata Division 1. akaenda kidato cha tano na sita hatimaye
Chuo kikuu cha Dodoma na sasa ana degree.
NI KWA SABABU ALITHUBUTU.
ALIZUNGUMZIA MAMBO MATATU YANAYOWEZA KUMTOA MTU KUTOKA SEHEMU MOJA HADI NYINGINE NA NDIO MAMBO YALIYOMTOA YEYE (ROSE)
1. DESIRE (SHAUKU KUU)
2. DETERMINATION (DHAMIRIO/KIU)
3. FAITH (IMANI)
Walihudhuria watu wa dini/imani tofautitofauti na ndio kusudio la semina hizi.
ANGALIA PICHA MBALI MBALI.
MUNGU AKUBARIKI, USIKOSE KUFIKA NCHI YA AHADI.
MCH. HARRIS
KAPIGA ATAKUWA AKITOA RATIBA ZAIDI KILA SIKU YA JUMAPILI KWENYE KIPINDI
CHA GOSPEL TRACK (G.T) AMBACHO KINAENDESHWA NA YEYE MWENYEWE KUPITIA
CLOUDS FM RADIO.
|
No comments:
Post a Comment