Pages

Sunday, August 11, 2013

AJALI....YA BASI LA MERIDIANI ENEO LA MBWEWE BASI LIMEKATIKA NA SITI ZIPO NJE.

Bai la Merdiani lililokuwa limetoka Rombo kwenda Dar. Limeanguka hapa karibu na mbwewe . Watu wamekufa. Basi limekatika siti zipo njee. Dereva bado hajatolewa. taarifa zinasema dereva wake kafia hapo hapo na abiria wengine pia wamefariki

Thursday, August 8, 2013

SEMINA YA UJASIRIAMALI NDANI YA NCHI YA AHADI NA MCH. HARRIS KAPIGA

.





MCH. HARRIS KAPIGA.
Wakati wengine wanatumia uwezo wa fursa ama elimu walizo nazo kujipatia kipato kwa wale wenye kuhitaji ujuzi wa kitu fulani, Ndani ya huduma ya NCHI YA AHADI, Sinza Kamanyola kuna semina na mafunzo ya ujasiriamali na yanatolewa bure bila malipo yeyote na ni kwa watu wa aina zote kwa maana ya watu wa Imani zote.

Jana tar. 12 Jan 2013 Blog hii ilifanikiwa kuhudhuria Semina hii. Ki ukweli ilikuwa nzuri sana pia kulikuwa na shuhuda nzuri sana za jinsi mtu alivyoweza KUTHUBUTI (Daring).

Abela na Robert (mkurugenzi) walikuwa wazungumzaji!


Abela akiwa anagonga nyundo.

Dada Abela alizungumzia takribani mambo matano ya msingi, somo lilibeba kichwa kisemacho '' JINSI YA KUJIENDELEZA KIFANI ''_ How can we develop our carrier!

1. TAMBUA KUSUDI LAKO DUNIANI.
2. MAONO YAKO DUNIANI NI NINI
3. UNAPENDELEZ NINI (VALUES/INTERESTS)
4. UNA HAIBA YA AINA GANI (PERSONALITY)
5. ANGALIA FURSA ZAKO (EXPLORE YOUR POSSIBILITIES)

Hivyo ni vidokezo tu (highlights) ya vile alivyofundisha na alifafanua kwa kina sana.

Robert naye aliachilia nyundo zake!

Alizungumzia mambo makuu ya msingi. Sitatoa maelezo bali nakupa dondoo tu ya kile alichozungumza. Ukitaka ufaidi vizuri unakaribishwa NCHI YA AHADI, Sinza Kamanyola; DSM

DONDOO/HIGHLIGHTS
1. KUJIAMINI
2. KUJIZUIA/KUWA NA NIDHAMU
3. UVUMILIVU.


Rose Tarimo alitoa ushuhuda wenye kujenga sana sio kusisimua!


Dada Rose Tarimo ni moja kati ya watu ambao wanastahili kufuatwa as a role modal. Huyu dada baada ya kumaliza elimu ya msingi alikaa nyumbani miaka nane lakini ndani yake alikuwa na shauku kuu ya kutaka kusoma wakati huo hana mtu wa kumsomesha!
Aliamua kukusanya madaftari ya wanafunzi wa sekondari na kuanza kujisomea mwenyewe bila ya mwalimu, baadae akanunua namba ya mtihani. Akafanya mtihani akapata Division 1. akaenda kidato cha tano na sita hatimaye Chuo kikuu cha Dodoma na sasa ana degree. 
NI KWA SABABU ALITHUBUTU.

ALIZUNGUMZIA MAMBO MATATU YANAYOWEZA KUMTOA MTU KUTOKA SEHEMU MOJA HADI NYINGINE NA NDIO MAMBO YALIYOMTOA YEYE (ROSE)

1. DESIRE (SHAUKU KUU)
2. DETERMINATION (DHAMIRIO/KIU)
3. FAITH (IMANI)

Walihudhuria watu wa dini/imani tofautitofauti na ndio kusudio la semina hizi.


ANGALIA PICHA MBALI MBALI.






















MUNGU AKUBARIKI, USIKOSE KUFIKA NCHI YA AHADI.
MCH. HARRIS KAPIGA ATAKUWA AKITOA RATIBA ZAIDI KILA SIKU YA JUMAPILI KWENYE KIPINDI CHA GOSPEL TRACK (G.T) AMBACHO KINAENDESHWA NA YEYE MWENYEWE KUPITIA CLOUDS FM RADIO.

CHRIS MAUKI AZUNGUMZA_TOFAUTI ZA KIJINSIA ZINAVYOWEZA KUATHIRI MAHUSIANO YETU.






 Mwanasaikolojia Chris Mauki azungumza ndani ya Nchi Ya Ahadi jinsi tofauti za kijinsia zinavyoweza kuathiri mahusiano yetu.





Siku zote dhana ya mahusiano inaweza kuwa na namna mbili tofauti kutokana na tofauti za jinsia zetu wenyewe. Lakini kwanza tujiulize nini maana ya MAHUSIANO?

Mahusiano_ Ni ujenzi wa uhusiano wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke unaohusisha sana hisia.

TUNAWEZA KUYAGAWANYA MAHUSIANO KATIKA MAKUNDI MANNE.

1> Kundi la watu walio katika mahusiano ya urafiki hadi uchumba.
2> Kundi la watu wanaoanza kujiunga/kujiingiza kwenye mahusiano.
3> Kundi la watu ambao tayari wako kwenye ndoa.
4> Kundi la watu ambao hawajajiingiza kwenye mahusiano kabisa.

TOFAUTI ZA KIJINSIA.

Mara nyingi kunaweza kuwa na tofauti mbalimbali kutokana na utofauti wa kijinsia unaotokana na chanzo au vyanzo mbalimbali vinavyoleta tofauti ambayo inatokana na Asili Yetu.
Asili yetu ni pale mmoja asemapo ''mimi ni mwanaume, yeye ni mwanamke''

VYANZO VYA TOFAUTI HIZI.

a) Malezi. 
Mara nyingi malezi ndiyo yanayoweza kuonyesha tabia asilia ambayo anayo mtu kulingana na jinsia yake. Wazazi ndio nyenzo kuu ya kumfanikisha mtoto kuwa na malezi bora yenye mtazamo mzuri wa kuwa na mahusiano mazuri kwa wazazi wenyewe na hata kwa jamii inayomzunguka.
Lazima wazazi watumie vyema fursa zao kuwajenga watoto wao katika misingi iliyo thabiti katika maisha yao yote.

b) Makuzi.
Katika hatua ya ukuaji mzazi ndiye amtengenezaye mtoto katika hatua zote za ukuaji wa kimwili na kiroho kutokana na umri wake.

Utafiti alioufanya Chris Mauki.

Katika utafiti wangu ( Chris Mauki), 2012 huko Afrika Ya Kusini imeonyesha kuwa familia nyingi huwa na mzazi mmoja (single parent family) ambapo watoto huwa chini ya uangalizi wa malezi ya mzazi mmoja, hivyo mtoto huathiriwa kisaikolojia zaidi.

Mfumo/aina za familia:
Familia ni mkusanyiko wa watu wenye uhusiano mmoja na kukaa pamoja.

Aina za familia.
-familia yenye mzazi mmoja na watoto (single parent family)
-familia yenye wazazi wawili (nuclear family)
-familia yenye wazazi, watoto na ndugu wengine (extended family)
-familia ambayo haina wazazi (non-parents family)

c) Watu wanaokuzunguka (marafiki).
Huenda marafiki au watu wanaokuzunguka ndio wanaoweza kuwa chanzo cha kuibua utofauti, kwani unaweza kusikia maneno yanayosemwa kwa kujadili mambo ambayo ni sumu kali ya kuibua tatizo katika jamii.

d) Maisha yako ya awali (life background).
Ujionavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo na ndivyo watu watakavyokuona. Maisha yako ya awali yanaweza kukupa swali la kujiuliza; 'jinsi ujionavyo nafsini mwako ndiyo chimbuko la kuibua furaha au huzuni maishani mwako'.

Matatizo ya kimahusiano:
Matatizo siku zote hutokana na namna mtu anavyoweza kujitengenezea mwenyewe.
Lakini matatizo ya kimahusiano watu wengi hushindwa kuyatatua kwa sababu ya kutokujua tofauti zao za kijinsia.

Mifano ya tofauti za kijinsia.
i> Wanawake wengi wameathiriwa na manunuzi (shopping) wakati wanaume hawazingatii sana manunuzi/shopping.

ii> Wanawake wengi hawazingatii sana mpangilio wa muda katika mipango yao. Lakini wanaume wengi huzingatia muda zaidi.

iii> Kwa matumizi ya pesa wanawake hutumia vibaya kuliko wanaume.

Nini tufanye kutatua tatizo?

- Lazima kila mtu aelewe chanzo cha tatizo na kulitatua
- Utayari wa kuchukuliana udhaifu
- Kuendana tabia.

JE! WANAWAKE WANASEMA NINI KWA WANAUME?
Kwa tafiti zilizofanywa nchini, imeonekana kuwa wanaume hawawezi kuelezea hisia zao walizo nazo kwa undani zaidi.

Wanaume pia hawana ukweli katika kuonyesha uhusiano zaidi.

Wanaume wengi wana fikra hasi kwa wanawake.

######################################################################

HAKIKA UHUSIANO BORA HUIBUA FURAHA MAISHA YOTE.

JINSI YA KUTATUA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO: AUNT SADAKA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA NA MAHUSIANO AZUNGUMZA.


     ''Watu wote duniani huwa tuna ndoto za kufanya kitu fulani lakini tumejikuta ndoto hizo
       hazijitokezi bayana kwa sababu ya kukosa UTHUBUTU''.

Migogoro ni ukinzani unaotokana na utofauti wa kiitikadi juu ya watu waaminio juu ya jambo fulani.
Mahusiano ni ukaribu wa watu ambao wana ushabihiano wa dhamira moja aidha dhamira ya kazi, au mapenzi mpaka ndoa.









Migogoro haiepukiki. Katika maisha lazima migogoro itokee kwa sababu ya mambo mbalimbali kama vile kitabia. Lakini wakati huo huo migogoro kwa wakati fulani ni mizuri kwani hutusaidia katika:

          * Kujitambua
          * Kujichuja kujua tabia ya mtu alivyo
          * Husaidia kujua msimamo wa mtu mwingine
          * Husaidia kuchomoza kwa mtu mwingine

Migogoro ya kimahusiano mahali pa kazi, familia na mapenzi hujitokeza na lazima itokee kila tunapokutana katika mzunguko wa maisha ya kila siku.

SABABU ZA MSINGI ZA MIGOGORO KATIKA MAPENZI NA KAZI:
1> Maeneo tutokayo na tuzaliwayo.
     Utofauti wa maeneo ni chanzo cha migogoro kwa sababu kila jamii au familia huzaliwa katika mitazamo 
     fulani, au uthamani fulani. Hivyo utofauti huo huleta migogoro.
Mfano: Mtu kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania hutofautiana kimtazamo, thamani na muonekano wake na aliyetoka mikoa ya kaskazini (Kilimanjaro), hivyo tukutanapo katika maeneo ya kazi na mapenzi huleta migongano awali kisha baadae hupoa.
   Hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kama umetoka katika familia inayoongozwa na upendo basi hata wafuasi
   wa familia hiyo kwa kiasi kikubwa wataongozwa na upendo, lakini mambo yakiwa kinyume na hapo
   basi kazini na hata katika mapenzi itakuwa Pakistani.
2> Muonekano (personality)
     Binadamu hutofautiana. Tumetofautiana katika maeneo makuu manne (katika mawasiliano).
# Namna tunavyotenda mambo yetu, katika kundi hili wapo wanaotenda mambo yao haraka wengine
   kwa wastani na wengine taratibu, hivyo hata katika mapenzi tofauti hizi hujitokeza.
# Tofauti katika mapenzi: Katika uga huu hutofautiana kwa kiasi kikubwa kwani wapo wanaopenda
   kubembelezwa na wale wasiopenda kubembelezwa, wengine wapo kimvuto zaidi na wengine  hapana.
# Masuala ya uchumi na fedha. Watu hutofautiana katika kupata fedha. Katika suala zima la kutunza  
   utumizi wa pesa, migogoro mingi katika familia nyingi Tanzania na duniani husababishwa na fedha kwani 
   watu hutofautiana. Wapo wanaojua kutafuta na kuzitumia fedha, wapo wanaozitafuta na wanakuwa
   wabahili wengine wanaweza kuzitafuta na watafunaji wazuri, Hivyo mtazame vyema mwenza wako na  
   umjue ili muweze kusuluhisha tatizo.
3> Matarajio (expectations)
     Jambo jingine linalosababisha migogoro katika maisha ya kimahusiano ya kikazi na katika kimapenzi ni
     matarajio. Watu wengi huwa na matarajio fulani lakini wengi wao wanapoingia na kukuta ndivyo sivyo
     na matarajio, huibuka migogoro.
Mfano kama unaomba kazi unategemea mshahara mzuri na kukuta sivyo, basi hapo ndipo mgogoro huibuka.
4> Kukosa Imani (lack of trust).
     Kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu katika maeneo ya kazi na mahusiano huzua migongano.
     Katika maeneo ya kazi uaminifu unapotoweka ndipo makundi na unafiki huibuka, pia katika mapenzi
     msipoaminiana lazima kutakuwa na migogoro. Kama miongoni mwenu kuna hisia kuwa unachezea timu 
     mbili basi utaibua mgogoro. Tambua kuwa katika maisha hakuna jambo zuri kama THAMANI; 
     Usimchukulie poa mpenzi wako. Daima elewa kuwa kupenda na kupendana ni kuonesha udhaifu ulio 
     nao kwa umpendaye. Katika mapenzi hakuna kuchukuliana poa.
     Tambua kuwa duniani kuna watu ambao huamini kuwa dunia inaweza kusimama kwa kupiga mluzi, yaani
     kila wanachokisema wao wako sawa na wana haki, watu wa aina hii wanapoingia katika mahusiano basi
     huwa ni hatari. Tabia hii ni heri akawa nayo mwanamme kuliko mwanamke.
5> Ubinafsi (selfishness)
     Watu wengi wana tabia ya ubinafsi hivyo wanasababisha migogoro katika mahusiano ya kimapenzi. 
     Hivyo unapokutana na mtu wa aina hii basi umeumia. Unaweza kuona umekosea na huwezi kuonekana
     kuwa hujui lolote. Watu wa aina hii hata ukimwambia... I MISS YOU...!
     Utasikia: kheeee! Leo umejifunza wapi?... Hivyo unaweza kuwa mtumwa, mwisho huchoka. Ipo athari 
     kama moyo uliopenda ukichoka hasa wa mwanamke kama vile:
@ Moyo wa mwanamke uchokapo ni kama bomu, kwa sababu huingiza maumivu na kutengeneza uvungu
     ambao hutengeneza bomu linalosubiriwa kulipuka.
@ Wanaume wao hubeba mambo, wanapotaka kulipuka hujulikana mapema.
@ Elewa uwekezaji mkubwa katika mapenzi kwa mwanamke ni hisia hivyo mwanamke anapoikosa basi
     hufanya chochote ili aipate. Hivyo wanaume wanatakiwa kuwatunza, kuwathamini na kuwajali vyema
     wake zao. Na uwekezaji mkubwa wa wanaume katika mapenzi ni hisia na fedha, daima moyo uwapo
     katika vuguvugu za kukosa amani basi utafanya ufujaji katika pesa kwa kununua vitu vya thamani ili
     kuitafuta amani iliyopotea, Je? Wanawake wangapi ambao wana magauni mapya ya thamani ambayo
     hayajavaliwa bado na wanaendelea kununua?
Tambua kuwa moyo uchokapo lazima utaingia katika DUARA la umasikini pia elewa kuwa vurugu vurugu za maisha zipo kila iitwapo leo, hivyo ukizikubali vurugu hizo zivunje miguu ya moyo wako utakuwa hoi kutumika.
VITU VYA KUFANYA ILI KUONDOKEWA NA MIGOGORO KATIKA MAPENZI NA KAZI:

Vipo vichocheo viwili ambavyo huweza kuondoa migogoro katika mapenzi na kazi, ambavyo ni:

a) Vitu tunavyoweza kufanya katika hatua yeyote ile (mahali popote)
b) Jinsi ya kutengeneza mahusiano (mapenzi) yenye afya.
Jambo muhimu daima ni kuwa tuingiapo katika mahusiano na kazi, kumpenda mtu hatutarajii kuumia na kuteseka. Yatafakari haya kwako na mengine hapo baadae.
Kisaikolojia hunenwa kuwa lazima uanze na wewe mwenyewe ndipo uende kwa mwingine. Watu wengi maishani hutumia muda mwingi kuwabadilisha wengine badala ya kuanza na wao wenyewe.
Hivyo uonapo hapo ulipo hapakufai anza kuleta mabadiliko wewe.
Vitu vya kufanya katika hatua yeyote ile:

  * Kuwa mtu mzima (grow up)
Hapa haina maana kuwa mtu mzima ni kuwa na ndevu (mabadiliko ya kibaiolojia), bali ni uwezo wa kusimamia mambo yako. Mtu mzima hahukumu watu wengine anapopatwa na migogoro. Mtu mzima hukubali makosa na kufikiria nafasi nyingine yenye usalama zaidi juu ya mahusiano yake.
  * Muombe Mungu akukuze, akupe busara na upeo.
Daima muombe Mungu akupe upeo na busara chanya ili uwe na uwezo wa kuchuja na kuacha mawazo mabaya. Elewa kuwa duniani watu waliofanikiwa ni wenye busara na upeo katika maamuzi yao.
  * Jikubali namna ulivyo.
Kwa bahati mbaya katika maisha wengi wetu hudanganya, na mpaka hujidanganya wao wenyewe. Katika kufanikiwa usijidanganye. Angalia mapungufu ulio nayo na uyafanyie kazi, kubali vitu usivyoviweza kisha fanyia kazi ili uweze.
  *Uwe tayari kujishusha.
Kuwa na tabia ya kuangalia na kusikiliza lakini si kwa kila kitu. Tambua siku zote kuwa ''kusikia si kuona na kuona si kweli''. Daima hakikisha kuwa unajua nini kinaendelea. Pia kuwa mnyenyekevu ingawa kitu kigumu duniani ni kuwa mnyenyekevu.
Watu wengi huona kuwa mtu mnyenyekevu ni mtu aliyeshindwa au ni muoga. Tambua kuwa kukubali ndio ushindi. Kwa nini ubishane?
Unyenyekevu katika mahusiano hususan katika mapenzi ni moja ya silaha  kuu ambayo itaufanya uhusiano wenu kuwa wa mfano. Daima unyenyekevu utawavusha katika mpando na mshuko wenu katika mahusiano. Mungu akiwapa neema hii (unyenyekevu) basi mtakuwa imara na wa mfano katika ndoa yenu.
b) Kichocheo cha pili.
Ni namna ya kujenga mahusiano yenye afya njema. Kila binadamu hupenda thamani yake ipande kila iitwapo leo lakini watu hushushana kila siku. Kila binadamu hupenda, hupendwa na kuthaminiwa.
MISINGI YA KUTENGENEZA MAHUSIANO YENYE AFYA.
a] Mkubali mpenzi wako.
Kama unahitaji kupendwa lazima umkubali mpenzi wako. Mtu anayemkubali mpenzi wake huyo hujiheshimu. Mtu anayejiheshimu hawezi kumdhalilisha mwingine kwani unapomdhalilisha hujidhalilisha mwenyewe.
b] Mheshimu na jiheshimu mwenyewe.
Mtu anayejiheshimu hatumii lugha chafu, huonesha heshima yake kuwa mwanzo wake. Hateremshi chupi ovyo ovyo.
c] Onesha mapenzi kwa kila hali.
Tambua kuwa unapompenda mtu hii humaanisha kuwa umemkubali na umekubali vitendo vyake, namna anavyosema n.k. Wasilisha upendo wako kwa namna zote iwe katika kuongea ama kushirikiana, kuweni marafiki. Neno samahani, ashakum si matusi.
Ngoja niulize kidogo.
'Ni nani yupo tayari kujamba mbele ya mpenzi wake?' (wote kimya)
Mkifikia hapa mjue mpo huru na mnapendana; ukiwa na hofu tambua kuwa hakuna upendo. Daima upendo huanzia machoni, kwenda kinywani, kisha huishia moyoni ambako hutulia tuliiii!!!!!. Bahati mbaya siku hizi mapenzi huanzia katika zipu au mfukoni.

d] Pokea na utoe mapenzi.
Ukiona kuwa wewe ni wa kutoa au kupokea mapenzi siku zote za mahusiano yenu basi unatakiwa uondoke mapema. Au anza upya.
e] Jipende mwenyewe.
Kumbuka kuwa huwezi kufanya mambo yote haya kama hujipendi wewe mwenyewe. Kama utajipenda wewe mwenyewe basi utajua namna ya kupenda. Ukimuona au ukisikia mtu anasema kuwa yuko tayari kufa kwa ajili yako huyu achana naye maana huweza kukuacha pia hata wewe ukitokwa na uhai. Pia kama mpenzi wako amekugeuza baba au mama basi achana naye. Omba Mungu akupe uwezo wa kumpenda na uwezo wa kuwa mkamilifu siku zote. Nyakati zote muombe Mungu, ukiwa katika unyenyekevu.
f] Daima muombe Mungu.
Daima omba Mungu kwani yeye hutuwazia mambo mema siku zote na majibu yake huwa ni ndiyo, si sasa na nina mawazo au mpango mzuri.
DONDOO MUHIMU:

// Uvumilivu katika mapenzi ni muhimu. Elewa kwa moyo uliopenda hauchoki wala kuhukumu, uko hai siku 
  zote.
// Unapoamua kumsamehe mtu samehe na kusahau. Na kama hujamsamehe kwa wakati huo mwambie ili 
   ajue na atafute mbinu m'badala ya kukuomba radhi.
// Zipo tabia ambazo hutokana na mazingira, kaeni chini muelimishane.
// Usione aibu katika mapenzi, elezaneni ukweli.
// Jifunzeni kutafuta chanzo na kiini cha tatizo.
// Ni vyema kuwa na mahusiano yenu binafsi. Pia kuelewa ndio jambo muhimu katika maisha.
// Usiingie katika mapenzi (mahusiano) kiupofu.
// Msome mwenzi wako.
// Mapenzi ni namna unavyomuonesha, unavyosema, matendo na ukifanyacho juu ya umpendaye. Fanyia kazi
   mahusiano yako.
// Pesa ni upendo siku zote. Usikubali kuingia katika mahusiano kwa sababu ya pesa.
// Mawasiliano ni muhimu. Muulize mpenzi wako namna anavyotaka apendwe na wewe .
// Nyumba ndogo ni hatari.
// Mtu anayependa kweli hachoki. Mtu hupenda mara moja.
// Usiingie ukurasa mpya wa mapenzi mapya kabla ya kuufunga wa awali.
// Elewa kusamehe na kusahau ndiyo nguzo ya mahusiano.
// Utandawazi usitufanye tuache mila na desturi za upendo wa kifamilia au kuwapeleka kwa bibi na babu.
// Mpenzi wako akifunga virago pengine anahitaji SAIKOLOJIA PUMZISHI (rest psychology) akizidi
   mueleze kuwa siku nyingine ukienda nitakuacha uende jumla.
// Msaidie kujaza imani iliyotoka juu ya mapenzi.
// Elewa kuwa watoto wana haki ya kuona baba na mama hata kam mkiachana