Pages

Wednesday, July 31, 2013

NAMNA YAKUMNASA MPENZI ANAYEKUFICHA TABIA ZAKE MBAYA


Tatizo ambalo limekuwa likiwakuta wapenzi wengi wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi wenye mwelekeo wa maisha ya ndoa ni kuingizwa ‘mkenge’ kwa kufichwa baadhi ya tabia mbaya na wapenzi wao.
Wapenzi wanaoficha tabia wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuteka mapezni ya watu, lakini baadaye wakishafanisha azma yao hujiachia na kuanza kuwatesa wenzao.
“Sikujua kabisa kama ana tabia hizi, ningetambua mapema kama ni mhuni nisingekubali kuoana naye.” 
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanandoa wengi mpaka sasa wanajuta kufunga ndoa na wapenzi wao na kwamba kama wangetambua tabia za wenza wao mapema wasingekubali kufunga ndoa.
Inawezekana hata wewe unayesoma makala haya unajuta kiasi cha kulalamikia mwenzako alivyobadilika tabia tofauti na mwanzo ulivyoanza kupendana naye. Hebu fuatilia dondoo hizi ili ujue namna ya kumtabua mpenzi anayekufichia makucha, ili usijiingize kwenye uhusiano usiokuwa sahihi.
MPE UHURU WA KUTOSHA
Watu wengi wanapoanzisha uhusiano huwabana sana wapenzi wao kwa kuwapekulia simu, kuwachunga watokapo na waingiapo, jambo ambalo huwafanya wahusika kujilinda sana wakiamini wanafuatiliwa.
Ndugu yangu usimbane mpenzi wako, mwache huru, atembee atakavyo na awasiliane na amtakaye, wewe kaa nyuma yake ukimchunguza bila mwenyewe kujua. “Mke/mume wangu hajali mambo haya” Hujali kumbe unamteka mwisho wa yote utamnasa. 
MPE MAJUKUMU
Ukisha mchagua umpendaye, huwezi kutambua uwezo wake mpaka umpe majukumu ya kufanya. Kwa mfano mtume akalipie maji, umeme au mwagize asimamie jambo fulani. 
Ukishafanya hivyo kaa kando mwangalie, anavyoiba chenji, anavyopunguza gharama bila kukushirikisha, lakini baadaye muulize, utashangaa alivyotibua mambo akidhani wewe si mtu wa kujali sana, kumbe ulikuwa umemtega na hatimaye umemnasa.
MUWEKE KWENYE WAKATI MGUMU
Njia nyingine ya kumnasa anayekufichia makucha ni kumweka katika wakati mgumu. Wanasema rafiki wa kweli hujulikana kwa dhiki. Tengeneza dhiki kwa makusudi na kuzitekeleza. Akikuambia naomba unitumie vocha mpenzi au ninunulie nguo mwambie sina pesa, halafu uone kama atakuwa na kiwango kile kile cha mapenzi. Wapo wanaume wengine wa pesa na mishahara ya wapenzi wao, ili kuwabaini ni kuwanyima wakati mwingine.
TUMIA WATU
Katika hali ya kawaida, majirani na marafiki wanawatambua zaidi wapenzi wetu kuliko jinsi tunavyowatambua sisi. Inawezekana kabisa mpenzi wako akawa mtakatifu unapokuwepo lakini ukiondoka anajiachia ile mbaya, hivyo ili kujua tabia zake waulize rafiki na jirani zako watakusaidia kumtabua mpenzi wako.
ANGALIA ANAVYOWATENDEA WENGINE
Wapenzi wengi wanapokuwa wamepata wapenzi hutazama wanavyotendewa wao na kudhani inatosha. Mtu muungwana huwatendea wengine mema. “Aa, mama naye kanichosha kila siku anataka pesa.” 
Hebu sikia kauli hii, kama mtu analalamika kuchoshwa na mama yake itakuwaje kwako? Amka na kutambua kuwa anakufichia makucha na ipo siku atakubadilikia hata wewe na kukutesa. Amka usikubali kudanganywa na mpenzi mnafiki.

Saturday, July 27, 2013

Choo Cha Gold Kilicho Nunuliwa Na Kanye West Na Kim Kardashian


Kwenye nyumba ya Kanye West Na Kim Kardashian yenye thamani ya dola Milioni 11 za Kimarekani kuna vitu vyenye thamani kubwa kama vitanda, jiko na makoche, ila kilicho make headline zaidi ni vyoo vyao vyenye thamani ya dola Milioni 1 za KiMarekani. Kwa mujibu wa HipHopWired.com, West na Kardashian wamenunua vyoo vinne vya Gold vyenye thamani ya dola milioni moja. Bonyeza Read More Uone Picha Zaidi


 
 

Wednesday, July 24, 2013

FIVE SIMPOLE RULES TO BE HAPPY....TARATIBU TANO ZA KUKU FANYA UWE MWENYE FURAHA.

1.free your heart from hatred

2.free your mind from worries

3.live simply

4.give more

5.demand less  expect miracles in life



no one can go back and make a brand new stat

anyone can start from now and make a brand new start endings....
god didn't  promise day without pain laughter without sorrow sun without rain but he did promise strength for the day comfort for the tears and light for the ways


disappointments are like road bumps the slow you down but you enjoy the smooth road  after wards don't stay on the bumps too long move on.



when you feel down because you didn't get what you want just sit tight and be happy because god has thought of something better to give you

when something happens to you good or bad consider what it means.

there's purpose to life's events, to teach you how to laugh more or not  to cry too hard

you cant make someone love you all you can do is be someone who can be loved the rest is up to the person to realize your worth

is better to lose your pride to the one you love than lose the one you love because of pride

we spend too much time looking for the  right person to love when or finding fault with those we already love when instead we should be perfecting the love we give

never abandon an old friend you will never find one who can take  his place friendship is like wine it gets  better us it grows older. when you have something in this five roles you can share what your friends on other social networks.

Jitambue.....SABABU MBOVU ZA KUINGIA KATIKA MAHUSIANO/NDOA (Fahamu kwanini wengi hujuta baada ta muda mfupi)

Lengo la kuingia kwenye ndoa, liwe zuri au liwe baya ndilo litakalotegemeza aina ya maisha yenu katika ndoa hiyo kuwa ya furaha au ya machungu. Baada tu ya kuoana na huyo mtu wako kwa sababu zisizo za msingi, siku, miezi au miaka siyo mingi utaanza kuchoka na kutamani kutoka nje ya hiyo ndoa kwa maana baina yenu hakuna muunganiko wa ndani (emotional attachment) baina ya wanandoa wawili. Na mara nyingi hali hii hupelekea msongo wa mawazo (stress), mfadhaiko wa moyo na kukosa furaha ndani ya ndoa. Na matokeo ya hali hii kumfanya mwanandoa mmoja au wote wawili kuanza kutafuta kutoshelezwa na kuliwazwa nje ya ndoa na hapa vinazaliwa vitu vingine kama uzinzi, kutengana, talaka au magomvi na mifarakano isiyoisha.

Wanandoa wengi hawajui nini wafanye, nini waelewe ili kufanya ndoa yao zifanikiwe. Thamani ya ndoa na jinsi ndoa inavyochukuliwa sikuhizi ni tofauti sana na nyakati za wazazi wetu, na hii imewafanya wengine kujikuta wako wenye ndoa kwasababu mbovu na hivyo ndoa nyingi kuvunjika au kuyumba baada ya muda mfupi tu. Vitu kama kudhamiria, heshima na uaminifu sio vya maana tena siku hizi, sababu watu wanaogopa kuonekana wazamani na washamba.

Mtazamo wa ulimengu juu ya ndoa umeharibiwa na magazeti, luninga na vitabu mbali mbali. Siku hizi kuishi bila ndoa ni kitu cha kawaida, kuwa na mpenzi nje ya ndoa sio kitu cha ajabu tena, mapenzi nje ya ndoa sio ya kushangaza hata kidogo. Kinyume chake ukionekana kuyashangaa haya, jamii itakushangaa wewe kwa jinsi ulivyo nyuma ya wakati. Mambo yamebadilika sana, zamani binti akikutwa bikira wakati anaolewa ilikuwa sifa kwake na familia nzima, siku hizi binti akikutwa bikira atachekwa, na watu kumshangaa wakihisi ana matatizo fulani. Hali kadhalika kwa kijana wa kiume aliyejitunza. Kwa bahati mbaya sana tunaishi katika jamii ya ajabu isiyoamini katika kujitoa kwa kweli na kudhamiria katika mahusiano. Jamii isiyoamini katika uaminifu, na ndiyo maana magomvi mengi hutokea pale simu ya mmoja inapoguswa. Kuwindana na kuchunguzana kumekuwa kawaida, maadili sio jambo la kuzingatiwa tena. Wanandoa wengi ni wale wenye majeraha ya moyoni na walio umizwa, kwa hiyo hutoka nje ya ndoa zao wakitafuta mwingine aliyeumizwa kama wao ili waliwazane.



1. Hofu ya umri kupita na kuzeeka
Wako wengi sana, hususani watu wa wajinsia ya kike ambao wamejikuta wakiwakubali wanaume wa aina yoyote ili mradi tu nao waolewe maana umri wao ulionekana kusonga sana na hofu ya kutoolewa kutanda. Mwanaume anayehusiana na mwanamke mwenye tabia hii huulizwa au kulazimishwa kila siku kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa binti au kutangaza ndoa. Ndoa nyingi za aina hii zimeishia kenye talaka na kutengana.

Wako wengine ambao kwasababu wanakiu sana ya kupata watoto na wameogopeshwa sana habari kwamba wana weza wasipate watoto kwa sababu ya umri wao, basi watacheka na kaka yeyote yule ilimradi tu waolewe au wazae naye. Wengine wajinsi hii wamejuta sana baada ya kujikuta kuwa waliyezaa naye hakuwa BABA bali mwanaume tu, tena kirukanjia tu na kwahiyo wanawake hawa wameishia kulea mtoto au watoto wao wenyewe pasipo mzazi wa pili (single parenting), jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linawaathiri watoto wengi. Kwa wale wanaokimbilia kuolewa ili wakazae watoto, kukumbuka kuwa hata huko kwenye ndoa kuna waliokosa watoto.



2. Kuingia katika ndoa/mahusiano kwa lengo la kusaidiwa au kuongeza kiwango cha kiuchumi ulicho nacho.
Hapa wengine wamewageuza wapenzi wao kuwa mitaji au rasilimali ya kuwaondoa wao pamoja na ndugu zao kutoka kwenye umasikini. Kwa kuthibitisha hili wengine wamepewa majina kama BUZI, ATM n.k.

Katika penzi la namna hii hakuna mguso au muunganiko wa kuhisia (intimacy) baina ya wapenzi, bali kinachowaunganisha pekee ni kile kilicho mfukoni au vile vinavyoshikika na kuonekana tu. Athari za penzi la aina hii lina fungua milango mingi kwa wahusika kutokuwa waaminifu na hata kujihusisha na mapenzi nje ya mahusiano yao.


3. Kuingia kwenye ndoa sababu ya mimba au mtoto aliyepatikana kabla ndoa
Lazima kutofautisha kuwa sababu iliyowapelekea kuzaa mtoto siyo itakayowapelekea kuoana. Acha sababu ya kuoana kwenu iwe penzi lenu la dhati na sio mimba au mtoto. Suala hili linahitaji pia wazazi wajue kwamba kitendo cha watoto kupeana mimba au kupata mtoto hakitoshi kuwa sababu ya kuwalazimisha kuoana, maranyingi wazazi wamewalazimisha watoto wao kuingia katika ndoa sababu ya mimba au mtoto na kujikuta wanawaharibia maisha yao mazima. Yanini kujiingiza katika mahusiano yakudumu kisa umempa au umepewa mimba na kuifanya hiyo ndio sababu ya kulazimisha muishi pamoja kama mume na mke wakati kabla ya mimba hiyo hakuna mmoja kati yenu aliyewahi kuwaza kuwa siku mmoja mtakuwa mume na mke, badala yake baada ya kipindi kifupi mnagundua kuwa hakuna penzi baina yenu bali kinacho waunganisha ni mtoto pekee. Maumivu na vikwazo baina yenu vinawadhihirishia wazi kuwa ninyi wawili hamkutakiwa kuwa pamoja bali mmelazimisha tu. Kinacho fuatia hapo ni kufungulia mlango penzi lingine nje au kufanya mkakati wa kusitisha mahusiano yenu ili kuitafuta furaha ya kweli sehemu nyingine.


4. Kulazimika kuingia kwenye ndoa au mahusiano ya kudumu kwasababu ya upweke, (Loneliness).
Mara nyingi mtu anapokuwa peke yake (single) huwaza kuwa ndoa ndiyo inayoweza kuwa utatuzi mkubwa wa matatizo yake. Nakubaliana na ukweli wa maandiko kwamba “Sio vema mtu awe peke yake…” lakini ni vizuri tukijua tofauti iliyopo baina ya kuwa peke yako na upweke. Hivi ni vitu viwili tofauti: kuwa peke yako inamaanisha kukosa mawasiliano au ukaribu na watu wengine, unakuwa kama uliyetengwa (being alone), wakati upweke (loneliness) inahusisha nafsi, akili na hisia (soul, mental and emotions) kuwa pweke au kujihisi kutengwa na hii ni ngumu kuishuhulikia. Ni heri kuwa peke yako (single) kuliko kuwa kwenye ndoa na bado ukajisikia upweke (lonely). Wako wengine waliodhani ndoa ni suluhisho la upweke waliokuwa nao na mara walipoolewa au kuoa, mawasiliano baina yao yakayumba na hivyo kukomaza upweke kwa wote wawili (Not alone but lonely).


5. Kuolewa au kuoa kwasababu ya shinikizo kutoka kwa wazazi, ndugu au marafiki
Shinikizo hizi zaweza kuwa za kihisia au hata kihalisia. Kihisia ni pale ndugu au wazazi wanapokushawishi mara kwa mara kuoa sababu umri wako unaonekana kwenda na wako wazazi wengine husisitiza kuwa wanataka wajukuu (utasikia mzazi anasema unataka nife sijawaona wajukuu zangu?). Hata kama huhisi kulazimishwa lakini kwa kule kurudia rudia kwa kukumbushwa kila siku kunaweka shinikizo ndani yako, kunaathiri hisia zako na kuweza kukupelekea kuingia katika ndoa isiyopangiliwa. Shinikizo la kimwili au kihalisia ni pale wazazi wanopolazimisha watoto wao kuoa au kuolewa na watu fulani kwa sababu tu ni marafiki zao (family friends) au kwa sababu ya kulinda utajiri na matarajio yoyote binafsi. Ndoa nyingi za aina hii zimekuwa kero na dimbwi la maumivu na machozi, baada ya muda kidogo mna jikuta mali mnazo, wazazi wenu wanapatana na kupendana, lakini nyie kama wapenzi ni maadui wakubwa. Jiulizeni mnaingia kwenye mahusiano kwa furaha yenu au ya wazazi wenu?


6. Kuamua kuoa au kuolewa ili kupata uhuru.
Hii hutokea sana kwa wale waliozoea kubanwa sana na wazazi katika kila wafanyacho hususani katika maamuzi. Wengine huzikimbia familia zao maana hazieleweki, hazina mpangilio na hivyo kutamani kutoka ili wakaanzishe zakwao wenyewe. Kinadada na kinakaka wanachoka kuamuliwa na kuwekewa masharti ya kuvaa, kula, kufanya mambo, kutoka na kurudi kwa muda kwahiyo wanadhani ndoa ndio itawachomoa kifungoni hapo. Ninaushahidi wakutosha wa baadhi ya ambao walikimbilia katika mahusiano ili kuwa huru na kwa bahati mbaya waliyoyakuta huko kwenye mahusiano yaliwafanya watamani hali waliyoiacha nyumbani kwao ingawa kwa bahati mbaya wakati huo ‘it was too late’.



Monday, July 22, 2013

FAHAMU JINSI YA KUISHI NA WATU WENYE TABIA YA KULAUMU

Hakuna hata mmoja anayependa kupokea lawama mara kwa mara, na mara nyingi inategemea ni jinsi gani unavyomjibu yule anayekulaumu, labda utamwambia maneno ya dharau kejeli, matusi au kujibu kihasira. Kibaya zaidi ni kwamba majibu haya yote hayampoozi mlaumu, kinyume chake yana mpa moto wa kuendelea kulaumu, na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.Katika hali zote lawama zinapotolewa kuna kiwango fulani cha upande mmoja kuhisi kutotendewa sawa, ingawa mara nyingine lawama hizi huelekezwa kwa asiye mhusika.Wengi hupenda kuzirusha lawama kwa wale walio dhaifu kwao, mfano. Baba kumlaumu mama, mama kulaumu watoto au wafanyakazi nk.Mara nyingi ni  ngumu kunyamaza pale unaporushiwa lawama, hususani pale unapojua kabisa kuwa lawama hizo hazikustahili wewe, katika hali kama hii yakubidi ujitahidi kukaa kimya, kwa sababu muhimu zifuatazo.
  1. Kama wote mtafuka moto na kuwajeuri au klujibizana hakuna kitakachofanyika, hali itakuwa ngumu zaidi na mlaumu au mlalamishi atapata kitu kingine cha kulaumu juu yako, yamkini akasema wewe huambiliki.
  1. Kwa vyovyote lawama zitakavyokuwa, fahamu tu  kuwa mteja (ikiwa ni kwenye biashara) wakati wote ana haki, fahamu hakuna biashara bila huyo mteja. Hata kama amekosa, mlaumu wakati wote hujiona ana haki ya kutoa malalamiko yake na kusikilizwa. Kwa kunyamaza na kumsikiliza, unatunza kazi yako na kuiendeleza.
  1. Kama kelele hazitapungua, lawama zaweza kuvuka mpaka na kuwa lawama au shutuma binafsi nahii yaweza kuleta ugomvi binafsi.
  1. Kwa sababu ni rahisi sana kupandishwa hasira zaidi ya kupooza hasira, ikiwa utamruhusu mlaumu akupandishe hasira, utalazimika kuzielekezea hata kwa watu wengine wasio husika, ambao unahitaji kuwapa huduma pia. Hii sio haki na inawapa mlango mwingine wa kuanza kukulaumu.
  1. Ukiruhusu mtu akupandishe hasira, kiwango chako cha msongo wa mawazo kitapanda, na hivyo waweza kujikuta unapata matatizo kiafya. Mfano. Kuumwa kichwa mara kwa mara, mgongo kuuma, mshtuko wa tumbo, na mapigo ya moyo kuzidi kasi. BP, wale wenye vidonda vya tumbo huzidi kuuma nk.
  1. Kuruhusu kupandiswa hasira mara kwa mara kazini, huwafanya wengi kwenda kuzishushia nyumbani, nah ii huleta mfarakano na watu wa kwenye familia. Hasira na migongano hii ikizidi nyumbani, kasi utalala na kuamka nayo na hivyo kwenda nayo kazini asubuhi, hii ukufanya kuanza siku na hasira na hivyo kukuaruzana na yeyote yule.
  1. Unajua kabisa kuwa, sio jukumu lako kukasirikia kazini dhidiya mteja au wale unaowahudumia, hali hii ikitokea, utajihisi vibaya moyoni, na waweza wapoteza hata wale ulionao karibu na walio marafiki.

NINI TUFANYE KWA MTU MWENYE TABIA YA LAWAMAJitahidi kujiweka huru, mpole na asiyepaniki kwa vyovyote iwezekanavyo (be relaxed as possible) vuta pumzi ndefu, acha mabega na shingo yako iwe huru mbali na hasira na jaribu kuhisi utulivu.Tulia hadi joto na moto wa mlaumu ushuke, ukijaribu kuweka neno hapa, atatulia na kukuamkia tena. Mwili wako uonyeshe mawasiliano, weka pozi la utulivu sio la shari, muangalie machoni, usimkwepe, kama ni kwenye meza, egemea kidogo upande wake kama vile uko tayari kumsikiliza kwa upole.Msikilize anachosema sawia, ikiwezekana chukua karatasi na kalamu akuone ukiandika pointi za kile anachalaumu. Hii itakusaidia kumwonyesha kuwa unamaanisha na hivyo kushuhulikia kile anacholaumu. Pia itakukumbusha wewe nini haswa kilikuwa kinalaumiwa mara baada ya yeye kunyamaza.Baada ya kusikiliza anachokisema, mwonyeshe mlaumu kuwa unahisi sawa na vile anavyojisikia, na hata ingekuwa niwewe ungeumia au ungelaumu pia. Mfano; Mwambie “Naelewa kabisa jinsi ilivyokuudhi hasa kwa jinsi ilivyotokea” hii inamwonyesha anayelaumu kuwa unamuhurumia na kwamba huoni kuwa analaumu tu bila sababu.Pata muda wa kuliangalia tatizo kiundani, sio mara zote mlaumu ana haki, ingawa hauhitaji kumwambia hivyo usoni kwake. Kama ni jambo litakalohitaji muda basi mwombe muda wa kulishuhulikia na muahidi kumpa taarifa baadaye na kweli ufanye hivyo ulivyoahidi.Pale unapogundua kuwa unamakosa katika lile lililokuwa lina laumiwa, basi kuwa mrahisi kuomba radhi na uwe mkweli usitake kufunika mambo na kujitetea.Kamwe usijitetee, hatakama sio wewe mhusika mfano; “Sio kosa langu” mimi sikuwepo jana” kamwone bosi basi “Usilaumu kabla ya kuuliza kwanza” nk. Mlaumu hana muda wa kujua nani ni mhusika ili amlaumu yeye. Ukitupia lawama kwa wengine kama ni kwenye ofisi au kampuni basi unafanya wateja au mteja kupoteza imani na ofisi au wafanyakazi wengine.Kinachotakiwa, fanya kile uwezacho kupunguza tatizo, na mlaumu akuone ukiwabize kulifanya hilo. Mara utakapo mweleza kuwa unafanya kitu basi akuone ukikifanya muda huo.Usishangae, hata mtu unaemjua kuwa ni mpole, anaweza kuwa mkali mara tu anapogeuka kuanza kuwa mtoalawama, na hasa kama sio mara ya kwanza kwa tatizo la jinsi hiyo kutokea. Ni ngumu kuanza tu kushuhulikia kila anachokilaumu kabla kwanza hauja shuhulikia hisia zake. Sungumza nae kwanza. Mruhusu amalize kuongea ili apoe. Tingisha kichwa taratibu kuonyesha uko na yeye, akimaliza ongea taratibu.

Lawama kwa njia ya simu:Katika hali hii, yakupasa ujitahidi kuwa mpole, hata kama hiyo simu inaingilia mambo na ratibu zako za kazi, najua hii ni ngumu hasa ukizingatia kuwa mlaumu hakuachii hata nafasi ya kumsikiliza, bali anafuka tu kama moto.Weka kalamu na karatasi karibu na wewe mara zote (kama ni ofisini) akiacha nafasi kidogo, muulize jina lake na ikibidi anapiga simu kutoka wapi, au ofisi gani, kama huna uhakika mwambie akutajie tarakimu za jina lake au la ofisi.Kama kuna kitu utalazimika kuangalia katika mafaili, vitabu au computer, basi muulize kama angependelea kusubiria katika simu (hold on) au angependa kukata simu na umpigie baada ya muda kidogo.
Kamwe usiweke mkono katika kisemeo (ikiwa ni simu ya mezani) mlaumu atajua kwamba umeamua kumfanyia ukatili na hutaki kumsikiliza. Hii ni kwa sababu simu za sasa zimetengenezwa katika hali ambayo sauti inapita sawa katika sehemu ya kuzungumza na sehemu ya kusikilizia.Ikiwa unataka kumkatisha mlaumu, wakati wote. Jaribu kumwita kwa jina lake, hii itamfanya atulie kukusikiliza zaidi ya kusema “samahani” “unajua”, ni kweli…..”Kama ni kitu ambacho hautaweza kukishuhulikia muda huo, muahidi kukishuhulikia baada ya muda fulani na ujitahidi kuwa mwaminifu katika ahadi yako na atarajie majibu ya kutia moyo. Mpe jina lako, pia, ili ajue ninani wa kuwasiliana nae ikiwa atahitaji kupiga simu tena. Hii itamjengea imani ya kuwa, unamaanisha kumsaidia. Hata kama bado mambo hayajamalizika basi umpigie katika muda ulioahidi ili kumpa ripoti ya kunachoendelea. Kama hautaweza kulishuhulikia wewe, basi muahidi kumpa mtu muafaka wa kumsaidia, nawewe uwe karibu kuhakikisha madai yake yanashuhulikiwa.
Labda kosa laweza kuwa lako, ikiwa hivi, basi kubali na kumtaka radhi, jaribu kumwelezea jinsi utakavyojitahidi kuweka mambo sawa, kamwe usijitetee wala kutupia lawama kwa wengine. Hali hii itakufanya uonekane dhaifu na mkwepa majukumu. Unapokubali na kushuka mara nyingi mlaumu nae huwa muelewa.Ikiwa unaona lawama zinakuwa kubwa na kushindwa kuzitafutia ufumbuzi haraka basi tafuta eneo au upenyo wa maafikiano, hii itafanya kasi ya ujeuri wa mlaumu kupungua kwasababu ni ngumu yeye kuendelea kupigizana kelele na mtu anae afiki kila usemalo.
 Lawama hizi za njia ya simu huwa zaidi katika ulimwengu wa biashara, lawama hizi huleta matatizo mengi zaidi.

Watu wengine ambao hawawezi kulaumu uso kwa uso, huwa rahisi kwa kutupa lawama kupitia simu. Katika biashara, au maofisini, hali huwa ngumu zaidi maana, unakuta mlaumu kashapiga simu kwa secretari (katibu muhtasi) nayeye akamruhusu mtu huyo aongee nawewe, basi anakuja na hasira mara dufu. Kama secretari sio mchapakazi na labda amechelewa kumuunganisha mlaumu huyu na wewe basi mlaumu anaweza kutakamani kukupasukia mara anapokupata wewe kwenye simu. Watu wengi huchemka zaidi kwenye simu zaidi ya wanavyokuwa ana kwa ana, hali hii hufanya maelewano kuwa magumu zaidi.

Kwa sababu hauwezi kuona sura ya huyo anayelaumu, wala mwili wake ni vigumu mmoja wenu kupoa maana haujui jinsi anavyojielezea au jinsi gani anamaanisha kutafuta suluhu.

KUNDI LA SCOPION GIRLZ KWISHA HABARI YAKE,SASA VIPANDE VIPANDE..WATUPIANA NGUO NJE


MEMBA wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wametofautiana hadi kufi kia hatua ya kutukanana na kutupiana nguo nje.
 

Mpango mzima ulitokea hivi karibuni Kijitonyama jijini Dar, nyumbani kwa Isabela ambapo chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Isabela kumsifi a mtandaoni X-memba wa kundi lao, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ kwa kununua gari, ndipo Kabula  alipokasirika na kuanza kumtukana Bela na mama yake matusi ya nguoni.
 

“Sikumuelewa kabisa Jini, kumsifi a Jack kuhusu kumiliki gari ndiyo kumemfanya anitukane? Iliniuma sana na sitamsamehe, bora kila mtu achukue hamsini zake, nguo zake nilimtupia nje,” alisema Bela na kusisitiza kufanya muziki peke yake kwa sasa

Friday, July 19, 2013

MAJAMBAZI WATEKA KITUO CHA POLISI

Hii imetokea huko Gongolamboto jana ,majambazi waliokuwa wamejihami kwa silaha za kisasa walivamia kituo Kidogo cha polisi kilichoko Gongolamboto na kuwateka polisi waliokuwemo kituoni humo na kuwafungia mahabusu ya kituo hicho, majambazi hao pia waliwajeruhi na walitaka silaha zaidi na radio call, hata hivyo walishindwa kwakuwa radiocall haikuwa na chaji(aibu nyingine ya jeshi la polisi) waliondoka wakiwaacha polisi ndani ya lockup yao mpaka walipokuja kuokolewa na wananchi
Source; Radio Wapo, Radio Tumaini

Wednesday, July 17, 2013

NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE COMPUTER YAKO.

Wengi wanalalama kuwa cm zao hazina whatsapp au wanashanga vipi mie napatikana kwenye hiyo mambo wakati na cm yangu ni ya Tochi tu.
Hebu cheki maelekezo  hapo chini ukimaliza kumbuka kuni Add na mimi ili tutumiane ma picha na mambo mengine….
Download App inaitwa Bluestack Kutoka hapa Run Mobile Apps on Windows PC or Mac with BlueStacks | Android App Player then Run Hyo app so Utakua na Access na Playstore so utaweza Kudownload App zote Ikiwemo Whatsapp Instagram, viber, tango, na nyingineee tu.

ila Hyo App Ni ina Mb 8 tu ila inahtaji Specs kubwaaa kwanza Ram Lazma Iwe 2gb Pia Graphic accelerator lazma ziwe Updated… So Kabla Ya Kudownload Na Kuinstall Fix Hzo kwanzaaa
Ukisha insall bluestack, ingia kwenye google play install go launcher ex, itaifanya hiyo bluestack iwe na mwonekano mzur wa android kama za cm, bt kunakua hakuna mwingiliano wwte kati ya pc na bluestack mfano ukitaka kutuma picha kwa kutumia watsapp na kama hiyo picha imo kwenye pc, inatakiwa ui install dropbox kwenye pc yako.
Kumbuka, youwave ni yakulipia (Ingawa unaweza kuichakachuwa) ila bluestack ni ya bure, isipokuwa ina ishu za ram, vga drivers etc.

NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE COMPUTER


Wengi wanalalama kuwa cm zao hazina whatsapp au wanashanga vipi mie napatikana kwenye hiyo mambo wakati na cm yangu ni ya Tochi tu.
Hebu cheki maelekezo  hapo chini ukimaliza kumbuka kuni Add na mimi ili tutumiane ma picha na mambo mengine….
Download App inaitwa Bluestack Kutoka hapa Run Mobile Apps on Windows PC or Mac with BlueStacks | Android App Player then Run Hyo app so Utakua na Access na Playstore so utaweza Kudownload App zote Ikiwemo Whatsapp Instagram, viber, tango, na nyingineee tu.

ila Hyo App Ni ina Mb 8 tu ila inahtaji Specs kubwaaa kwanza Ram Lazma Iwe 2gb Pia Graphic accelerator lazma ziwe Updated… So Kabla Ya Kudownload Na Kuinstall Fix Hzo kwanzaaa
Ukisha insall bluestack, ingia kwenye google play install go launcher ex, itaifanya hiyo bluestack iwe na mwonekano mzur wa android kama za cm, bt kunakua hakuna mwingiliano wwte kati ya pc na bluestack mfano ukitaka kutuma picha kwa kutumia watsapp na kama hiyo picha imo kwenye pc, inatakiwa ui install dropbox kwenye pc yako.
Kumbuka, youwave ni yakulipia (Ingawa unaweza kuichakachuwa) ila bluestack ni ya bure, isipokuwa ina ishu za ram, vga drivers etc.

Jitambue Ya Chris Mauki....ALAMA 11 ZA KUKUONYESHA KUWA MPENZI WAKO SIO MWAMINIFU (some signs of cheating)



7. Mabadiliko katika tendo la ndoa:
Jambo hili laweza kujidhihirisha katika picha mbili tofauti. Kwa kawaida wapenzi huwa na mazoea fulani katika tendo la ndoa, kwa muda waliokaa pamoja kila mmoja humfahamu mwenzake kwa kiasi fulani. Inawezekana likawa jambo la kushangaza pale ambapo gafla unamuona mpenzi wako anapoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa, au hata mnapokuwa katika tendo hilo humuoni akifurahia bali anakuwa kama anayelazimishwa au kutohamasishwa na chochote. Kwa upande mwingine unaweza ukakuta mpenzi wako anakuja na ujuzi wa gafla katika mahusiano yenu ya tendo landoa, hali yake ya kukutamani inazidi gafla, anahitaji mapenzi mara kwa mara na hata mnapokuwa katika tendo hilo anadhihirisha utaalamu wa tofauti na ule uliouzoea. Hali hizi mbili zifanyike tahadhari katika kukusaidia kuyatazama mahusiano yenu.

8. Marafiki wa mpenzi wako kukukwepa:
Ni hali yakawaida kuwa karibu au kuzoeana na marafiki wa mpenzi wako, maranyingine mtawasiliana nao kutaka kujua aliko mpenzi wako au kinachoendelea kwao. Inabidi ujiulize sana pale inapotokea gafla wale marafiki wa mpenzi wako uliowazoea, uliokuwa unawapigia simu wakati wowote leo wana kukwepa, na hata simu hawapokei na maranyingine wakipokea hawakupi taarifa yakueleweka au wanakudanganya. Hii yote inawezekana wanamlinda rafikiyao, au wanakosa cha kujibu maana wanajua uhalisia wa kinachoendelea.


9. Kuzungumza sentensi za kutatanisha:
Kama nilivyosema awali, wapenzi wengi hujuana kwa mengi, 
ikiwemo pia namna ya kuzungumza au kuonyesha hisia. Unaweza kukuta katika mapenzi yenu mpenzi wako anaanza kuwa na sentensi ngumu na zisizo kuwa na msingi kwa mfano anasema “kwa jinsi hii sidhani kama tutafika” “mi siamini kama mapenzi yanadumu” “yani ndio maana watu wanashindwa kukaa na mpenzi mmoja” na maranyingine anaweza kukuuliza baadhi ya maswali moja kwa moja ili kukuona utajibuje. Sentensi hizi zina chanzo moyoni, kuwa macho.

10. Kuzidi kwa tabia za kutoonekana au kuponyoka:
Yawezekana mpenzi wako alikuwa na tabia ya kuwepo nyumbani mida isiyokuwa ya kazini au wikiendi, muda mwingi alipenda kuwa na wewe na akiaga basi atasema anakwenda wapi na akimaliza hurudi mapema kwa sababu anakiu ya kuwa nawewe, mara gafla sikuhizi haagi anakwenda wapi, ukiuliza inawezakuwa vita. Anakuwa na vijisafari vingi na vijisababu visivyoisha vya kumuwezesha kuponyoka. Sehemu ya kwenda na kurudi lisaa limoja anaweza kuchukua nusu siku, kila ukiuliza atakwambia nakuja, niko njiani, kuna foleni, nimekwama, na sababu nyingine nyingi sana. Ukiona haya yanazidi ujue kuna la zaidi ya foleni, na hizo sababu zote zinazotolewa zinafunika jambo.


11. Tabia za kuficha fedha:
Ninafahamu fika kwamba suala la uwazi katika mambo yanayohusiana na fedha na matumizi ni tatizo kubwa kwa wapenzi wengi, wengi wamegombana na hata kuachana kuhusiana na jambo hili. Japokuwa hili ni tatizo kwa wengi lakini wako wapenzi ambao wamekuwa na tabia ya kuambiana kwa uwazi matumizi na mapato yao, hakuna kitu wamefanya kuhusu fedha zao pasipo kuambiana na hivi ndivyo mlivyozoeshana, mara ghafla mmoja anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwa ulizwa kuhusu suala hilo. Tabia hii ikidhihirika katika mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana kwa kukaa kimya unaweza kujikuta umechelea mwana na maji ya moto.

HONGERA KWA WALE WALIOKUWEPO DARASANI KUANZIA MWANZO WASOMO HADI MWISHO. KWA WALE WALIOKOSA BASI TEMBELEENI samsasali.blogspot.com na shereheyetu.blogspot.com mtasoma alama zote huko.

SOMO LINALOKUJA:

ALAMA ZA KUKUONYESHA KUWA MPENZI WAKO ANATABIA ZA KIDIKTETA NA ANAKIU YA KUKUTAWALA
(IDENTIFY YOUR PATNER’S DOMINEERING BEHAVIOURS)

Saturday, July 13, 2013

Jitambue Ya Chris Mauki...FAHAMU JINSI YA KUISHUHULIKIA NA KUIPUNGUZA HOFU--Part 1


Hofu na mashaka ndio adui namba moja anayefilisi nguvu au nishati ya mwili wa mwanadamu kwa haraka kuliko kitu kingine chochote kile.  Wengi wameathiriwa katika maisha yao ya kielimu, kiafya, kijamii, kikazi na hata kiuchumi kwasababu ya  hofu au mashaka.

Wengi wameshindwa kufikia malengo na ndoto zao katika Maisha kwasababu ya hofu na mashaka.

Mara tu hofu na mashaka yanapoota ndani ya mtu hudumu kwa muda mrefu huku yakileta uharibifu mkubwa katika nafasi, akili, na maendeleo ya mtu huyo kwa ujumla.  Makala au mada  hii itakuwezesha kufahamu kwa kiasi kikubwa mambo unayoweza kufanya ili kuondokana au kupunguza athari za hofu na mashaka na pia kuweza kutoa msaada kwa yeyote anayepitia tatizo hili kwa wakati fulani.

Hofu ni mjumuiko wa kujali kusiko na  sababu yoyote (unnecessary concern) au kusiko na maana yoyote juu ya nafsi au utu wa mtu.  Tunasema  hakuna sababu wala umuhimu wowote kwa sababu kujali huku kumejengwa katika misingi ifuatavyo
-         Mtu kujali sana au kuweka  mawazo sana katika vitu ambavyo viko nje ya uwezo wake.
-         Mtu kuanza  kusikitikia mambo yajayo badala ya kujipanga na kujiandaa kuyakabili pale  yatakapo wadia.
-         Kuweka msisitizo zaidi katika jambo moja na kuyasahau mengine. Anayehofu hudhani kwamba ikiwa kile anachokiwekea msisitizo kitashindikana, basi kila kitu kitakuwa kimeharibika.
-         Mtu kushindwa kutumainia imani aliyonayo  juu ya ufanisi wa jambo fulani.  Hofu yake katika jambo fulani huizidi imani aliyonayo na kwahivyo  hali ya kushindwa kuonekana  dhahiri zaidi kuliko hali ya kushinda.

Kwasababu hofu hujengwa katika fikra  zisizo na maana wala uhalisi wowote, basi njia ya kuiweza hofu hiyo ni lazima  iwe kwa kutumia fikra zenye maana na uhalisi ili kuushinda uwezo wako wa kufikiri kushindwa.
Yafuatayo yatakusaidia kukuwezesha kupunguza kiwango cha hofu katika Maisha.

1.           Jiulize swali “Je nini kinachoniangamiza?”
Hofu ni kitu kinacho angamiza, tena huangamiza kwa viwango na hatua tofauti.  Ngoja nijaribu kukupa mfano wa maelezo.
Hofu kwa lugha ya kingereza ni “worry” neno “worry” limetokana na lugha ya Kidachi lenye  maana ya “Worgen”.  Maana ya neno “worgen” ukiipeleka moja kwa moja katika lugha ya kingereza humaanisha “strangle”. Maana ya neno “strangle” kwa lugha ya kiswahili ni “Kunyonga kwa kamba”. Sasa yamkini hapa unanielewa kwanini ninasema hofu huua au kuangamiza.

Uzuri ni kwamba, hofu haiangamizi pasipo kutoa tahadhari kabla,  baadhi ya tahadhari zinazotolewa katika mchakato wa kuangamizwa  na hofu ni pamoja na hamaki za mara kwa mara, mvi za mapema, baadhi ua upele fulani wa ngozi, vidonda vya tumbo (ulcers), matatizo ya kukosa usingizi, kuhitaji kwenda haja ndogo mara kwa mara n.k.

Swali hili la “ni nini kinachoniangamiza?” litakuwezesha kujitathmini wewe mwenyewe. Katika kulijibu swali hili utaweza kutathmini kwa kujiuliza kuwa “Ni nini katika maisha yangu ambacho nimekipa kipaumbele zaidi kuliko afya yangu na Maisha yangu?  Maana ya swali hili ni ukweli  kwamba kama unahofu katika jambo fulani maana yake hilo jambo au hicho kitu umekipa umuhimu au uzito usiostahili kuliko maisha yako.  Je ni jambo gani au  kitu gani umekipa umuhimu au uzito usiostahili katika maisha yako.  Je ni kazi yako?,  Je ni elimu yako? Je ni ujenzi wa nyumba?  Je ni kibali kwa watu? Je ni watoto wako au mwenza wako?  Je ni malipo ya mkopo uliouchukua? Kumbuka haitakufaidia wala kukuongezea chochote kwa kujiua ukikiwaza hicho kitu, mwisho wasiku mwenye  hasara ni wewe.

Hata mwisho  kama hautapoteza maisha yako lakini ukadhoofisha afya yako, faida yake nini nini?  Na afya yako ikipotea, nini tena utakifanya kuyanufaisha maisha yako?

Kama hofu yako ni kwenye kupata kibali machoni pa watu wanaokuzunguka, labda ofisini, chuoni, mtaani nk.  Kumbuka kuwa watu hao wala hawatajali au kukukumbuka pale utakapokuwa unaugulia wodini au nyumbani kwako kisa ni magonjwa yanayohusiana na hofu.
Labda mfano huu waweza kukusaidia zaidi kuelewa ninacho maanisha.
 Mtu mmoja kijana alimuuliza swali mwanafalsafa (philosopher) mmoja akisema, “Nini kinachokushangaza sana kwa huyu kiumbe binadamu?”

Mwanafalsafa alijibu “Ninamshangaa sana kiumbe mwanadamu kwa sababu hupoteza afya yake kwa kiasi kikubwa sana  akitafuta pesa, na baadae hutumia pesa yake yote akiitibu au kujaribu kuirejesha afya yake iliyo potea katika hofu za Maisha.  Kwa kuihofia kesho yake, mwanadamu huyu ametumia muda wote wa sasa akijiandaa na hiyo kesho, na matokeo yake, kwa kuichosha sana afya yake ameshindwa kuifurahia leo yake na hata hiyo kesho yenyewe huiona kwa taabu sana” (Mwenye ufahamu na afahamu).

 
1.     Acha kuyapa mawazo yako au mitazamo yako umuhimu usiostahili
Hofu, woga na hamaki za mara kwa mara ni alama kwamba unayapa mawazo, fikira na mitazamo yako umuhimu usiostahili.  Maana yake ni kwamba kila unaloliwaza au kulifikiri unalichukulia kua ni halisi, ingawa maranyingine ukweli ni kwamba unavyowaza sivyo.

Hakuna ukweli wala  uthibitisho kuwa kila unacho kiwazakitatokea.
Hizi twaweza kuziita fikra laini, pale ambapo unadhani kuwa kila unachowaza kitatolea.  Mtu mwenye ukichaa, akiwaza kuwa kuna mtu anataka kumpiga risasi atakimbia huku na huko kujificha. Wakati ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho. Wewe sio kichaa, kwanini uweke vyote unavyoviwaza  kama vile ni dhahiri? tena hususani vile vitu vibaya?

Tabia sugu nyingi walizonazo watu husababishwa na fikra, vile wanavyowaza.  Usiruhusu mawazo yako yakufanye mtumwa.  Mawazo ya kitaalam yanaonyesha kwamba kama ukiweka  mawazo yako sana katika kitu fulani, inaweza kuishawishi tabia au utendaji wako katika hali  ambayo yaweza kuanza kufanya hofu zako kuanza kuwa kweli. Ni kwasababu hii ndiyo maana, unashauriwa kuweka  mawazo na fikra zako zote kwenye vitu ambvyo ni vya maana.

2.     Usijiogopeshe kwa vitu ambavyo hutokea kwa nadra sana
Njia bora ya kuyatengeneza mawazo yetu yanayofikiri sana juu ya hatari ambazo kutokea kwa nadra sana ni kwa kuwaza kuwa wewe hautakuwepo pale hatari hiyo itakapo tokea katika eneo hilo, na hivyo haitakuathiri.

Kwanini uwaze kwamba wewe  una bahati mbaya  sana na vyote vibaya vitakapotokea vitakukuta wewe tu.  Najua inawezekama  kabisa lakini nafasi za kuwezekana huko ni ndogo sana.  Mfano. Kwanini uwaze kuwa unapotembea msituni peke yako, mti unaweza kukuangukia.  Au unapokukwa kwenye ndege au meli, ajali yaweza kutokea, au hata unapokuwa safarini kwa gari, jiulize mabasi mangapi yametoka kule unakotokea na kufika salama kule unakokwenda bila shida yeyote, wewe je huwezi kuwa mmoja wa waliokuwa salama?

Kuna mambo mengi ya kuogopesha yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku, na kama ukiogopa na kuhofu kila kitu na kutofuata ushauri unaotolewa hapa, basi kila siku utatembea na kuishi kwa hofu tu.

MASIKITIKO:MCHUMBA WA NEY WA MITEGO AANGUKA, MIMBA YACHOROPOKA


Rapper Nay wa Mitego leo anasherehekea siku ya kuzaliwa ya mchumba wake aliyekuwa mjamzito kwa huzuni kubwa baada ya mchumba wake huyo kukipoteza kichanga chao kufuatia kuanguka jana usiku.

“Jana usiku mke wangu alianguka, alifikia tumbo kwahiyo akawa anasikia kizunguzungu nilipompeleka hospitali daktari akasema mtoto amekufa,” Nay
Awali, Nay wa Mitego ameweka picha ya mchumba wake kwenye Instagram akiwa hospitali na kuandika: Happy bday my lv, Mungu akupe maisha marefu na yenye mafanikio tele. Japo imekukuta uko vibaya tumempoteza kijacho bt ni mipango ya mungu, nakupenda sana mke..!! #966# happy bday 2u ma.”

JE WEWE UPO KATIKA KUNDI LIPI KATI YA HAYA? JITAMBUE.


Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za

binadamu na hatimaye wamewagawanya
katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni

1. Introvant: watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina

hapa kuna makundi mawili
1.Melancolin 2. Fragmetic

2. extrovants: wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao
Hapa kuna makundi mawili
1. Sanguine 2. Colerick



Na sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao

1.MELANCOLIN
Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo
-wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligency Quetient)
-ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
-wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
-ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
-wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
-Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji --wanamaombi wazuri sana kiimani)
-Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
-Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
-Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
-Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasanu si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
-Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
-Wakata tamaa wanapokosolewa.
-Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
-Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
-Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo
-Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
-Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
-Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)
-Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
-Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana
-Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe
-Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
-Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
-Wana busara na hekima nyingi
-Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
-Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
-Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
-Ni kundi la watu wanoridhika haraka
-Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa
-Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
-Kundi linalopenda amani na utulivu
-Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
-Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu
-Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
-Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
-Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
-Wakati mwingine hupenda kujikataa.
-Ni waaminifu na wasema ukweli
-Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
-Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
-Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
-Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
-kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tama mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani]
-Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
-Kwa upamnde wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua


Mifano ya watu wa kundi hili: Musa (wa biblia) Yesu Kristo, Bob Marley, Celin Dion


2: FLAGMETIC
-Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
-Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini
-Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalili shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia)
-Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
-Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao
-Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea
-Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
-Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili
-Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hatawaliwa na mifano na takwimu halisia
-Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu)
-Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili
-Ni watu wasioumizwa kufanya makosa
-Hawapendi kuwaamini wenzao
-Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali
-Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
-Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao)
-Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
-Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka)
-Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea
-Si watu wanaojali muda na ratiba
-Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
-Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani
-Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
-Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)
-Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani
-Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu)
-Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko
-Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
-Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
-Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote
-Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao.
-Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia
-Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.


3.SANGUINE
-Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo)
-Ni wacheshi sana
-Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea
-Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza
-Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine
-Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili
-Wanapenda sana kujisifu na kujikweza
-Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia
-Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
-Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa uhakika
-Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
-Muda wote wako nadhifu (ni wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu)
-Wana kiherehere sana.
-Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau
-Ni vinyonga katika tabia zao (wanuwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua wasiwagundue kirahisi)
-Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi kuyaacha
-Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi
-Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja: __inasemekana kutokana na maneno yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.)
-Wawapo kwenye jamii hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao.
-Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha
-Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi
-Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama za kuhubiri kwa mvuto na ushawishi wa pekee)
-Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo
-Ni kundi la watu waoga sana (wanajiamini sana kwa maneno lakini kivitendo ni kunguru)
-Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji)
-Wanapenda kujaribu kila jambo linalokuja mbele yao
-Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
-Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine
-Hawana aibu hata mbele ya watu wasiowafahamu wala kuwazoea
-Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
-Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama madini)
-Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi)
-Ni watu wa mipango isiyoona mbali (wakurupukaji) (Ministers of emmergency affairs)
-Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kirahisi na kwa dhati)
-Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
-Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
Mfano ni Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kiti (alipomwona Yesu anatembea juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu (aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri (aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa (alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa)



1. COLERICK

-Wana uwezo wa kawaida kiakili
-Ni wa wakali na wakaidi
-Hawana huruma wala unyenyekevu
-Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
-Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
-Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa
-Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
-Watu wasiokata tamaa mapema
-Wanajiamini kupita kiasi
-Hawana uoga ni majasiri sana
-Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
-Kundi la watu wenye nguvu nyingi
-Ni madikteta
-Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
-Watu wa kulipiza visasi
-Watu wa vitendo kuliko maneno
-Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
-Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
-Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
-Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo -wa kiukandamizaji
-Hawajui kubembeleza
-Hawaongei wala kucheka ovyo
-Wanapotenda jambo huwa wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya kurudishiwa hicho alichokitoa
-Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa hasara
-Si watu wanaopenda suluhu na amani
-Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
-Hawapendi starehe kwa wingi
-Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki na shida
-Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
-Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha
-Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd Amin, Hitler, etc

*SI TABIA ZOTE ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA



MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU
-Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani
-Huwezi kujibadilisha kundi
-Kujifahamu kundi lako kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kuwa makini namna ya kuishi nao
-Inawezekana kabisa kujifahamu upo kundi gani na pia kwa kusoma na kutazama ni rahisi kutambua makundi ya wengine



*NITATAMBUAJE MIMI NI WA KUNDI GANI?
-Watu wengi wana tabia za makundi zaidi ya moja
-Kwa wale tabia zaidi ya asilimia themenini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure (i.e pure sanguine etc)
-Kama una tabia kutoka kundi zaidi ya moja, unaunganisha majina ya makundi mawili yenye tabia nyingi zaidi, unaanza jina la lile lenye asilimia nyingi zaidi
*Mfan
*Mfano: flag-coleick; cole-flagmetic, flag-colerick , sangu-melancolic, melanco-sanguine: etc
Uchambuzi huu umeandaliwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali ikiwemo, vitabu, tovuti, semina, makongamano.

SAIKOLOGIA'''''''''''''ZIJUE TABIA SABA ZAKUEPUKA ILI UWEZE KUFANIKIWA


Kama kuna mtu ambaye amekuwa akisoma makala zangu tangu nilipoanza kuandika na amekuwa akipenda kufanikiwa kimaisha namuomba kwa unyenyekevu, asiwe miongoni mwa watu ambao watakuwa na tabia zifuatzo kwani haweza kufanikiwa kimaisha.
Hufikiri, kusema na kufanya yasiwezekana

Watu wasioweza kufanikiwa hujaa fikra za kutofanikiwa na mara nyingi hulalamikia sana matatizo yao. Wakati mwingine wasioweza kufanikiwa hugeuza mambo mema na kuyafanya yaonekane mabaya, jua likiwaka watalalamika joto, likipoa watalaumu baridi, watalaumu foleni za barabarani, yaani kwao kila jambo wataligeuza na kulipa sababu mbaya. Hata wanaposhindwa kutekeleza jambo hutoa sababu, yote ni kuzilinda fikara zao za kutofanikiwa.
Tabia hii hukua mpaka kufikia hatua wanapowatazama wenzao hudhani kuwa wanawasengenya, kuwafanyia mambo mabaya, kuwasaliti, ilimradi tu ni kuwa kinyume na mambo mema. Watu wa namna hii hata kama watasaidiwa namna gani hugeuza misaada hiyo kuwa ya kujipendekeza na mara nyingi hupuuza wema haraka na kueneza mabaya ya mtu. Lakini pamoja na yote kutokana na fikra zao kuwa za kushindwa watu wa tabia hii hukata tamaa mapema, pale wanapofanya jambo na kuonekana lina ugumu kidogo.
Hutenda kabla ya kufikiri
Tabia ya pili ya watu wasioweza kufanikiwa kimaisha ni hii ya kutenda jambo kabla ya kufikiria. Watu wa aina hii, kuwa wepesi sana kununua vitu barabarani mara tu wanaposhawashiwa na macho au wauzaji. Utakuta mtu bila hata kujiuliza faida za kitu hicho anaamua haraka kukipata. Ataamua kwa haraka kuoa, kuolewa, kukubali kujiingiza katika mapenzi na hata kufanya jambo lo lote bila kujiuliza atanufaika vipi?
Hupenda kuzungumza zaidi ya kusikiliza

Watu ambao wako katika hatari ya kutofanikiwa ni wale ambao daima ni wazuri katika kuzungumza kuliko kusikiliza. Wao huwa ni wajuajia wa kila kitu, hawako tayari kupokea ushauri. Siku zote wanapokuwa kwenye makundi ya watu pengine wajuzi zaidi yao wao huwa hodari kujenga hoja kutetea mambo yao hata kama hayafai. Unaweza kumkuta mtu ni kiongozi wa ngazi za juu, amefanya kosa na watu wote wameona kuwa kakosea lakini mhusika hujiona si mikosaji.
Mtu anapokuwa muongeaji sana huwa mgumu kupokea ushauri wa ye yote, anachoamua yeye hukifanya kwa imani kuwa kinafaa. Ukiwa mtu mwenya tabia ya aina hii huwezi kufanikiwa kabisa katika maisha yako. Watafiti wa masuala ya biashara ulimwengini waliwahi kushauri kuwa mipango mizuri ya kibiashara hutoka kwa watu masikini, ambao walisema hufikiri zaidi namna ya kujikomboa kuliko matajiri wanavyofikiri katika kujiendeleza, hivyo wakasema kama mtu anataka kufanikiwa kibiashara lazima asikilize mawazo ya masikini si kuwapuuza kwa kujiona ni bora zaidi yao.
Hukata tamaa mapema
Watu wanaotaka kufanikiwa huchukulia ushindwa kama hatua ya kuelekea kwenye mafanikio, lakini watu wasioweza kufanikiwa wanapojaribu mara moja au mbili kuvuka kikwazo fulani cha kimaisha na kushindwa hukata tamaa na kutotaka kujaribu tena kusonga mbele. Wanye tabia ya kushindwa kimaisha hawako tayari kudumu na jambo moja linaloonekana kushindikana kwao kwa muda mrefu. Akiona mwanamke ambaye ni mkorofi kidogo, haraka hukimbilia kumwacha na kutafuta mwingine, mara nyingi si watu wavumilivu.
Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi, anaaza kupika maadazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi ilimradi ni kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha. Ukitaka kuwa mmoja kati ya watu wasiweza kufanikiwa kimaisha, basi jaribu kuishi maisha ya kukata tamaa mapema unapofanya mambo.
Hujaribu kuwarudisha nyuma wengine
Wasioweza kufanikiwa katika maisha huwa na tabia moja ya ajabu ambayo ilianzishwa na Hawa mwanamke anayetajwa katika Kitabu cha Biblia kuwa ni mtu wa kwanza kufanya dhambi. Mwanamke huyu alipodanganywa na nyoka na kuchuma tunda hakutosheka na dhambi zake, bali alimpelekea na mumewe Adamu naye akala. Mara nyingi watu walioshindwa kimaisha kuwa na tabia za kuwashawishi watu wengine wawe kama wao katika mawazo na matendo.
Tabia za watu wa aina hii huwa si za kimaendelezo kwa vile wao hudhani kuwa njia zao ni sahihi na hivyo hujaribu kwa nguvu zao kuwarudisha wengine nyuma ili wawe kama wao. Ni watu wenye wivu wa ‘kijinga’ wakiona mwingine anaendelea katika hiki na kile humpiga vita ili afilisike. Ni wingi wa fitina, uchonganishi. Wenye tabia za kutofanikiwa hudhani kuwa kukwama kwao hutokana na vikwazo vinavyoletwa na wengine. “Kwa sababu jamaa kanikwamisha hiki na kile, nimkwama kwa sababu ya kaka yangu”
Hupoteza muda mwingi
Watu ambao hawawezi kufanikiwa ni wale ambao hupoteza muda mwingi kufanya mambo yasiyokuwa na tija, kwa kuangalia Tv, kusengenya watu, kunywa pombe, kufanya starehe na kutumia muda hovyo kwenye kazi ambazo hazina msaada kwao. Wapo watu mahodari kutembelea kwenye nyumba za wengine na kuongea huko kutwa nzima bila kujali kama muda waliopoteza wangeweza kufanya kazi na kujipatia kipato.
Huchagua mambo rahisi
Wakati mwingine mafanikio huhitaji kufanya kazi ngumu zenye kuchosha, lakini watu wasiokuwa na uwezo wa kufanikiwa wanapoletewa mambo mawilii huwa wepesi zaidi kuchagua jepesi kulifanya. Kama ni kazi, basi zisiwe ngumu sana ziwe nyepesi nyepesi ambazo watazifanya bila jasho. Watu wasiokuwa kwenye njia ya mafanikio hawapendi kujituma, wepesi kuchoka na mara nyingi hupenda sana kufanya kazi kidogo na kulala sana.
Tabia za watu wasioweza kufanikiwa huwa ni za kukwepa kuwajibika. Hata kama kuna mtu anataka kumpatia kitu na akamwambia awahi kesho yake asubuhi, huchelewa kwa vile hawezi kujihimu asubuhi na kuacha raha ya usingizi, wakati mwingine hata akiambiwa asubiri mpaka muda fulani huwa hayuko tayari kusubiri.
Leo naomba niishie hapa, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi. Kwa mtu mwenye shida tuwasiliane kwa email richmanyota@yahoo.com .