MADAM, Wema Sepetu ameonesha upande wa pili wa maisha yake baada ya kunaswa akikata mauno mwanzo mwisho.
Kwa
mujibu wa mtandao mmoja wa Kibongo, Madam alifi ka na kampani yake
katika Ukumbi wa Thai Village, Masaki jijini Dar hivi karibuni na ndipo
‘mashetani’ yalipompanda baada ya kusikia sebene lililokuwa
likiporomoshwa na Bendi ya Skylight.
Wema...
Pages
Tuesday, September 10, 2013
Madawa ya Kulevya: Matumla na Kaniki wakamatwa!
Jana kuna habari tulikuwa tunaisoma hapa juu ya mchezaj wa simba kukamatwa na unga Italy, ila habari yenyewe ilikua inatiliwa mashaka kwa sababu hata location hazikua sawa.
Leo kwenye gazeti la mwananchi wameripoti kuwa Mkwanda Matumla na Joseph Kaniki 'Golota' wamekamatwa na dawa za Kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, mjini Adis Abab, Ethiopia.
=================
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.
Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.
Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.
Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).
Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika
la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha
jana kwamba wanamichezo hao wanashikiliwa nchini humo na Polisi wa
Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
Wanamichezo hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakamu Kuu ya
Ethiopia iliyoko kwenye eneo la Arada, Addis Ababa kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu.
Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu.
Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
Alisema uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
“Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10 sasa, sisi tulipigiwa
simu na polisi wa hapa Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna
Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na Matumla,” alisema Shelukindo.
“Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na huo mzigo
walipewa na mtu mmoja. Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa anajuana vizuri na Mkwanda. “Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu.
Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi
Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe. Walipofika hapa Mkwanda
alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo
akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine
ilikuwa ya Mkwanda.
“Ndipo hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege wakashikiliwa na
Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano (kesho) na uchunguzi wa polisi bado unaendelea.”
Wanamichezo hao walidai kwamba walikabidhiwa mizigo hiyo kwenye
Uwanja wa Ndege wa Mombasa walipokuwa wakikabidhiwa pasi za
kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Ki...y/-/index.html
Sunday, August 11, 2013
AJALI....YA BASI LA MERIDIANI ENEO LA MBWEWE BASI LIMEKATIKA NA SITI ZIPO NJE.
Bai la Merdiani lililokuwa limetoka Rombo kwenda Dar. Limeanguka hapa karibu na mbwewe . Watu wamekufa. Basi limekatika siti zipo njee. Dereva bado hajatolewa. taarifa zinasema dereva wake kafia hapo hapo na abiria wengine pia wamefariki
Thursday, August 8, 2013
SEMINA YA UJASIRIAMALI NDANI YA NCHI YA AHADI NA MCH. HARRIS KAPIGA
.
MCH. HARRIS KAPIGA. |
Jana tar. 12 Jan 2013 Blog hii ilifanikiwa kuhudhuria Semina hii. Ki ukweli ilikuwa nzuri sana pia kulikuwa na shuhuda nzuri sana za jinsi mtu alivyoweza KUTHUBUTI (Daring).
Abela na Robert (mkurugenzi) walikuwa wazungumzaji!
CHRIS MAUKI AZUNGUMZA_TOFAUTI ZA KIJINSIA ZINAVYOWEZA KUATHIRI MAHUSIANO YETU.
Mwanasaikolojia Chris Mauki azungumza ndani ya Nchi Ya Ahadi jinsi tofauti za kijinsia zinavyoweza kuathiri mahusiano yetu.
Siku zote dhana ya mahusiano inaweza kuwa na namna mbili tofauti kutokana na tofauti za jinsia zetu wenyewe. Lakini kwanza tujiulize nini maana ya MAHUSIANO?
Mahusiano_ Ni ujenzi wa uhusiano wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke unaohusisha sana hisia.
TUNAWEZA KUYAGAWANYA MAHUSIANO KATIKA MAKUNDI MANNE.
1> Kundi la watu walio katika mahusiano ya urafiki hadi uchumba.
2> Kundi la watu wanaoanza kujiunga/kujiingiza kwenye mahusiano.
3> Kundi la watu ambao tayari wako kwenye ndoa.
4> Kundi la watu ambao hawajajiingiza kwenye mahusiano kabisa.
TOFAUTI ZA KIJINSIA.
Mara nyingi kunaweza kuwa na tofauti mbalimbali kutokana na utofauti wa kijinsia unaotokana na chanzo au vyanzo mbalimbali vinavyoleta tofauti ambayo inatokana na Asili Yetu.
Asili yetu ni pale mmoja asemapo ''mimi ni mwanaume, yeye ni mwanamke''
VYANZO VYA TOFAUTI HIZI.
a) Malezi.
Mara nyingi malezi ndiyo yanayoweza kuonyesha tabia asilia ambayo anayo mtu kulingana na jinsia yake. Wazazi ndio nyenzo kuu ya kumfanikisha mtoto kuwa na malezi bora yenye mtazamo mzuri wa kuwa na mahusiano mazuri kwa wazazi wenyewe na hata kwa jamii inayomzunguka.
Lazima wazazi watumie vyema fursa zao kuwajenga watoto wao katika misingi iliyo thabiti katika maisha yao yote.
b) Makuzi.
Katika hatua ya ukuaji mzazi ndiye amtengenezaye mtoto katika hatua zote za ukuaji wa kimwili na kiroho kutokana na umri wake.
Utafiti alioufanya Chris Mauki.
Katika utafiti wangu ( Chris Mauki), 2012 huko Afrika Ya Kusini imeonyesha kuwa familia nyingi huwa na mzazi mmoja (single parent family) ambapo watoto huwa chini ya uangalizi wa malezi ya mzazi mmoja, hivyo mtoto huathiriwa kisaikolojia zaidi.
Mfumo/aina za familia:
Familia ni mkusanyiko wa watu wenye uhusiano mmoja na kukaa pamoja.
Aina za familia.
-familia yenye mzazi mmoja na watoto (single parent family)
-familia yenye wazazi wawili (nuclear family)
-familia yenye wazazi, watoto na ndugu wengine (extended family)
-familia ambayo haina wazazi (non-parents family)
c) Watu wanaokuzunguka (marafiki).
Huenda marafiki au watu wanaokuzunguka ndio wanaoweza kuwa chanzo cha kuibua utofauti, kwani unaweza kusikia maneno yanayosemwa kwa kujadili mambo ambayo ni sumu kali ya kuibua tatizo katika jamii.
d) Maisha yako ya awali (life background).
Ujionavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo na ndivyo watu watakavyokuona. Maisha yako ya awali yanaweza kukupa swali la kujiuliza; 'jinsi ujionavyo nafsini mwako ndiyo chimbuko la kuibua furaha au huzuni maishani mwako'.
Matatizo ya kimahusiano:
Matatizo siku zote hutokana na namna mtu anavyoweza kujitengenezea mwenyewe.
Lakini matatizo ya kimahusiano watu wengi hushindwa kuyatatua kwa sababu ya kutokujua tofauti zao za kijinsia.
Mifano ya tofauti za kijinsia.
i> Wanawake wengi wameathiriwa na manunuzi (shopping) wakati wanaume hawazingatii sana manunuzi/shopping.
ii> Wanawake wengi hawazingatii sana mpangilio wa muda katika mipango yao. Lakini wanaume wengi huzingatia muda zaidi.
iii> Kwa matumizi ya pesa wanawake hutumia vibaya kuliko wanaume.
Nini tufanye kutatua tatizo?
- Lazima kila mtu aelewe chanzo cha tatizo na kulitatua
- Utayari wa kuchukuliana udhaifu
- Kuendana tabia.
JE! WANAWAKE WANASEMA NINI KWA WANAUME?
Kwa tafiti zilizofanywa nchini, imeonekana kuwa wanaume hawawezi kuelezea hisia zao walizo nazo kwa undani zaidi.
Wanaume pia hawana ukweli katika kuonyesha uhusiano zaidi.
Wanaume wengi wana fikra hasi kwa wanawake.
######################################################################
HAKIKA UHUSIANO BORA HUIBUA FURAHA MAISHA YOTE.
JINSI YA KUTATUA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO: AUNT SADAKA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA NA MAHUSIANO AZUNGUMZA.
''Watu wote duniani huwa tuna ndoto za kufanya kitu fulani lakini tumejikuta ndoto hizo
hazijitokezi bayana kwa sababu ya kukosa UTHUBUTU''.
Migogoro ni ukinzani unaotokana na utofauti wa kiitikadi juu ya watu waaminio juu ya jambo fulani.
Mahusiano ni ukaribu wa watu ambao wana ushabihiano wa dhamira moja aidha dhamira ya kazi, au mapenzi mpaka ndoa.
Migogoro haiepukiki. Katika maisha lazima migogoro itokee kwa sababu ya mambo mbalimbali kama vile kitabia. Lakini wakati huo huo migogoro kwa wakati fulani ni mizuri kwani hutusaidia katika:
* Kujitambua
* Kujichuja kujua tabia ya mtu alivyo
* Husaidia kujua msimamo wa mtu mwingine
* Husaidia kuchomoza kwa mtu mwingine
Migogoro ya kimahusiano mahali pa kazi, familia na mapenzi hujitokeza na lazima itokee kila tunapokutana katika mzunguko wa maisha ya kila siku.
hazijitokezi bayana kwa sababu ya kukosa UTHUBUTU''.
Migogoro ni ukinzani unaotokana na utofauti wa kiitikadi juu ya watu waaminio juu ya jambo fulani.
Mahusiano ni ukaribu wa watu ambao wana ushabihiano wa dhamira moja aidha dhamira ya kazi, au mapenzi mpaka ndoa.
Migogoro haiepukiki. Katika maisha lazima migogoro itokee kwa sababu ya mambo mbalimbali kama vile kitabia. Lakini wakati huo huo migogoro kwa wakati fulani ni mizuri kwani hutusaidia katika:
* Kujitambua
* Kujichuja kujua tabia ya mtu alivyo
* Husaidia kujua msimamo wa mtu mwingine
* Husaidia kuchomoza kwa mtu mwingine
Migogoro ya kimahusiano mahali pa kazi, familia na mapenzi hujitokeza na lazima itokee kila tunapokutana katika mzunguko wa maisha ya kila siku.
SABABU ZA MSINGI ZA MIGOGORO KATIKA MAPENZI NA KAZI:
1> Maeneo tutokayo na tuzaliwayo.
Utofauti wa maeneo ni chanzo cha migogoro kwa sababu kila jamii au familia huzaliwa katika mitazamo
fulani, au uthamani fulani. Hivyo utofauti huo huleta migogoro.
Mfano: Mtu kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania hutofautiana kimtazamo,
thamani na muonekano wake na aliyetoka mikoa ya kaskazini (Kilimanjaro),
hivyo tukutanapo katika maeneo ya kazi na mapenzi huleta migongano
awali kisha baadae hupoa.
Hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kama umetoka katika familia inayoongozwa na upendo basi hata wafuasi
wa familia hiyo kwa kiasi kikubwa wataongozwa na upendo, lakini mambo yakiwa kinyume na hapo
basi kazini na hata katika mapenzi itakuwa Pakistani.
2> Muonekano (personality)
Binadamu hutofautiana. Tumetofautiana katika maeneo makuu manne (katika mawasiliano).
# Namna tunavyotenda mambo yetu, katika kundi hili wapo wanaotenda mambo yao haraka wengine
kwa wastani na wengine taratibu, hivyo hata katika mapenzi tofauti hizi hujitokeza.
# Tofauti katika mapenzi: Katika uga huu hutofautiana kwa kiasi kikubwa kwani wapo wanaopenda
kubembelezwa na wale wasiopenda kubembelezwa, wengine wapo kimvuto zaidi na wengine hapana.
# Masuala ya uchumi na fedha. Watu hutofautiana katika kupata fedha. Katika suala zima la kutunza
utumizi wa pesa, migogoro mingi katika familia nyingi Tanzania na duniani husababishwa na fedha kwani
watu hutofautiana. Wapo wanaojua kutafuta na kuzitumia fedha, wapo wanaozitafuta na wanakuwa
wabahili wengine wanaweza kuzitafuta na watafunaji wazuri, Hivyo mtazame vyema mwenza wako na
umjue ili muweze kusuluhisha tatizo.
3> Matarajio (expectations)
Jambo jingine linalosababisha migogoro katika maisha ya kimahusiano ya kikazi na katika kimapenzi ni
matarajio. Watu wengi huwa na matarajio fulani lakini wengi wao wanapoingia na kukuta ndivyo sivyo
na matarajio, huibuka migogoro.
Mfano kama unaomba kazi unategemea mshahara mzuri na kukuta sivyo, basi hapo ndipo mgogoro huibuka.
4> Kukosa Imani (lack of trust).
Kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu katika maeneo ya kazi na mahusiano huzua migongano.
Katika maeneo ya kazi uaminifu unapotoweka ndipo makundi na unafiki huibuka, pia katika mapenzi
msipoaminiana lazima kutakuwa na migogoro. Kama miongoni mwenu kuna hisia kuwa unachezea timu
mbili basi utaibua mgogoro. Tambua kuwa katika maisha hakuna jambo zuri kama THAMANI;
Usimchukulie poa mpenzi wako. Daima elewa kuwa kupenda na kupendana ni kuonesha udhaifu ulio
nao kwa umpendaye. Katika mapenzi hakuna kuchukuliana poa.
Tambua kuwa duniani kuna watu ambao huamini kuwa dunia inaweza kusimama kwa kupiga mluzi, yaani
kila wanachokisema wao wako sawa na wana haki, watu wa aina hii wanapoingia katika mahusiano basi
huwa ni hatari. Tabia hii ni heri akawa nayo mwanamme kuliko mwanamke.
5> Ubinafsi (selfishness)
Watu wengi wana tabia ya ubinafsi hivyo wanasababisha migogoro katika mahusiano ya kimapenzi.
Hivyo unapokutana na mtu wa aina hii basi umeumia. Unaweza kuona umekosea na huwezi kuonekana
kuwa hujui lolote. Watu wa aina hii hata ukimwambia... I MISS YOU...!
Utasikia: kheeee! Leo umejifunza wapi?... Hivyo unaweza kuwa mtumwa, mwisho huchoka. Ipo athari
kama moyo uliopenda ukichoka hasa wa mwanamke kama vile:
@ Moyo wa mwanamke uchokapo ni kama bomu, kwa sababu huingiza maumivu na kutengeneza uvungu
ambao hutengeneza bomu linalosubiriwa kulipuka.
@ Wanaume wao hubeba mambo, wanapotaka kulipuka hujulikana mapema.
@ Elewa uwekezaji mkubwa katika mapenzi kwa mwanamke ni hisia hivyo mwanamke anapoikosa basi
hufanya chochote ili aipate. Hivyo wanaume wanatakiwa kuwatunza, kuwathamini na kuwajali vyema
wake zao. Na uwekezaji mkubwa wa wanaume katika mapenzi ni hisia na fedha, daima moyo uwapo
katika vuguvugu za kukosa amani basi utafanya ufujaji katika pesa kwa kununua vitu vya thamani ili
kuitafuta amani iliyopotea, Je? Wanawake wangapi ambao wana magauni mapya ya thamani ambayo
hayajavaliwa bado na wanaendelea kununua?
Tambua kuwa moyo uchokapo lazima utaingia katika DUARA la
umasikini pia elewa kuwa vurugu vurugu za maisha zipo kila iitwapo leo,
hivyo ukizikubali vurugu hizo zivunje miguu ya moyo wako utakuwa hoi
kutumika.
VITU VYA KUFANYA ILI KUONDOKEWA NA MIGOGORO KATIKA MAPENZI NA KAZI:
Vipo vichocheo viwili ambavyo huweza kuondoa migogoro katika mapenzi na kazi, ambavyo ni:
a) Vitu tunavyoweza kufanya katika hatua yeyote ile (mahali popote)
b) Jinsi ya kutengeneza mahusiano (mapenzi) yenye afya.
Jambo muhimu daima ni kuwa tuingiapo katika mahusiano na kazi, kumpenda
mtu hatutarajii kuumia na kuteseka. Yatafakari haya kwako na mengine
hapo baadae.
Kisaikolojia hunenwa kuwa lazima uanze na wewe mwenyewe ndipo uende kwa
mwingine. Watu wengi maishani hutumia muda mwingi kuwabadilisha wengine
badala ya kuanza na wao wenyewe.
Hivyo uonapo hapo ulipo hapakufai anza kuleta mabadiliko wewe.
Vitu vya kufanya katika hatua yeyote ile:
* Kuwa mtu mzima (grow up)
Hapa haina maana kuwa mtu mzima ni kuwa na ndevu (mabadiliko ya
kibaiolojia), bali ni uwezo wa kusimamia mambo yako. Mtu mzima hahukumu
watu wengine anapopatwa na migogoro. Mtu mzima hukubali makosa na
kufikiria nafasi nyingine yenye usalama zaidi juu ya mahusiano yake.
* Muombe Mungu akukuze, akupe busara na upeo.
Daima muombe Mungu akupe upeo na busara chanya ili uwe na uwezo wa
kuchuja na kuacha mawazo mabaya. Elewa kuwa duniani watu waliofanikiwa
ni wenye busara na upeo katika maamuzi yao.
* Jikubali namna ulivyo.
Kwa bahati mbaya katika maisha wengi wetu hudanganya, na mpaka
hujidanganya wao wenyewe. Katika kufanikiwa usijidanganye. Angalia
mapungufu ulio nayo na uyafanyie kazi, kubali vitu usivyoviweza kisha
fanyia kazi ili uweze.
*Uwe tayari kujishusha.
Kuwa na tabia ya kuangalia na kusikiliza lakini si kwa kila kitu. Tambua siku zote kuwa ''kusikia si kuona na kuona si kweli''. Daima hakikisha kuwa unajua nini kinaendelea. Pia kuwa mnyenyekevu ingawa kitu kigumu duniani ni kuwa mnyenyekevu.
Watu wengi huona kuwa mtu mnyenyekevu ni mtu aliyeshindwa au ni muoga. Tambua kuwa kukubali ndio ushindi. Kwa nini ubishane?
Unyenyekevu katika mahusiano hususan katika mapenzi ni moja ya silaha kuu ambayo itaufanya uhusiano wenu kuwa wa mfano. Daima
unyenyekevu utawavusha katika mpando na mshuko wenu katika mahusiano.
Mungu akiwapa neema hii (unyenyekevu) basi mtakuwa imara na wa mfano
katika ndoa yenu.
b) Kichocheo cha pili.
Ni namna ya kujenga mahusiano yenye afya njema. Kila binadamu hupenda
thamani yake ipande kila iitwapo leo lakini watu hushushana kila siku.
Kila binadamu hupenda, hupendwa na kuthaminiwa.
MISINGI YA KUTENGENEZA MAHUSIANO YENYE AFYA.
a] Mkubali mpenzi wako.
Kama unahitaji kupendwa lazima umkubali mpenzi wako. Mtu anayemkubali
mpenzi wake huyo hujiheshimu. Mtu anayejiheshimu hawezi kumdhalilisha
mwingine kwani unapomdhalilisha hujidhalilisha mwenyewe.
b] Mheshimu na jiheshimu mwenyewe.
Mtu anayejiheshimu hatumii lugha chafu, huonesha heshima yake kuwa mwanzo wake. Hateremshi chupi ovyo ovyo.
c] Onesha mapenzi kwa kila hali.
Tambua kuwa unapompenda mtu hii humaanisha kuwa umemkubali na umekubali
vitendo vyake, namna anavyosema n.k. Wasilisha upendo wako kwa namna
zote iwe katika kuongea ama kushirikiana, kuweni marafiki. Neno
samahani, ashakum si matusi.
Ngoja niulize kidogo.
'Ni nani yupo tayari kujamba mbele ya mpenzi wake?' (wote kimya)
Mkifikia hapa mjue mpo huru na mnapendana; ukiwa na hofu tambua kuwa
hakuna upendo. Daima upendo huanzia machoni, kwenda kinywani, kisha
huishia moyoni ambako hutulia tuliiii!!!!!. Bahati mbaya siku hizi
mapenzi huanzia katika zipu au mfukoni.
d] Pokea na utoe mapenzi.
Ukiona kuwa wewe ni wa kutoa au kupokea mapenzi siku zote za mahusiano yenu basi unatakiwa uondoke mapema. Au anza upya.
e] Jipende mwenyewe.
Kumbuka kuwa huwezi kufanya mambo yote haya kama hujipendi wewe
mwenyewe. Kama utajipenda wewe mwenyewe basi utajua namna ya kupenda.
Ukimuona au ukisikia mtu anasema kuwa yuko tayari kufa kwa ajili yako
huyu achana naye maana huweza kukuacha pia hata wewe ukitokwa na uhai.
Pia kama mpenzi wako amekugeuza baba au mama basi achana naye. Omba
Mungu akupe uwezo wa kumpenda na uwezo wa kuwa mkamilifu siku zote.
Nyakati zote muombe Mungu, ukiwa katika unyenyekevu.
f] Daima muombe Mungu.
Daima omba Mungu kwani yeye hutuwazia mambo mema siku zote na majibu yake huwa ni ndiyo, si sasa na nina mawazo au mpango mzuri.
DONDOO MUHIMU:
// Uvumilivu katika mapenzi ni muhimu. Elewa kwa moyo uliopenda hauchoki wala kuhukumu, uko hai siku
zote.
// Unapoamua kumsamehe mtu samehe na kusahau. Na kama hujamsamehe kwa wakati huo mwambie ili
ajue na atafute mbinu m'badala ya kukuomba radhi.
// Zipo tabia ambazo hutokana na mazingira, kaeni chini muelimishane.
// Usione aibu katika mapenzi, elezaneni ukweli.
// Jifunzeni kutafuta chanzo na kiini cha tatizo.
// Ni vyema kuwa na mahusiano yenu binafsi. Pia kuelewa ndio jambo muhimu katika maisha.
// Usiingie katika mapenzi (mahusiano) kiupofu.
// Msome mwenzi wako.
// Mapenzi ni namna unavyomuonesha, unavyosema, matendo na ukifanyacho juu ya umpendaye. Fanyia kazi
mahusiano yako.
// Pesa ni upendo siku zote. Usikubali kuingia katika mahusiano kwa sababu ya pesa.
// Mawasiliano ni muhimu. Muulize mpenzi wako namna anavyotaka apendwe na wewe .
// Nyumba ndogo ni hatari.
// Mtu anayependa kweli hachoki. Mtu hupenda mara moja.
// Usiingie ukurasa mpya wa mapenzi mapya kabla ya kuufunga wa awali.
// Elewa kusamehe na kusahau ndiyo nguzo ya mahusiano.
// Utandawazi usitufanye tuache mila na desturi za upendo wa kifamilia au kuwapeleka kwa bibi na babu.
// Mpenzi wako akifunga virago pengine anahitaji SAIKOLOJIA PUMZISHI (rest psychology) akizidi
mueleze kuwa siku nyingine ukienda nitakuacha uende jumla.
// Msaidie kujaza imani iliyotoka juu ya mapenzi.
// Elewa kuwa watoto wana haki ya kuona baba na mama hata kam mkiachana
Wednesday, July 31, 2013
NAMNA YAKUMNASA MPENZI ANAYEKUFICHA TABIA ZAKE MBAYA
Wapenzi wanaoficha tabia wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuteka mapezni ya watu, lakini baadaye wakishafanisha azma yao hujiachia na kuanza kuwatesa wenzao.
“Sikujua kabisa kama ana tabia hizi, ningetambua mapema kama ni mhuni nisingekubali kuoana naye.”
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanandoa wengi mpaka sasa wanajuta kufunga ndoa na wapenzi wao na kwamba kama wangetambua tabia za wenza wao mapema wasingekubali kufunga ndoa.
Inawezekana hata wewe unayesoma makala haya unajuta kiasi cha kulalamikia mwenzako alivyobadilika tabia tofauti na mwanzo ulivyoanza kupendana naye. Hebu fuatilia dondoo hizi ili ujue namna ya kumtabua mpenzi anayekufichia makucha, ili usijiingize kwenye uhusiano usiokuwa sahihi.
MPE UHURU WA KUTOSHA
Watu wengi wanapoanzisha uhusiano huwabana sana wapenzi wao kwa kuwapekulia simu, kuwachunga watokapo na waingiapo, jambo ambalo huwafanya wahusika kujilinda sana wakiamini wanafuatiliwa.
Ndugu yangu usimbane mpenzi wako, mwache huru, atembee atakavyo na awasiliane na amtakaye, wewe kaa nyuma yake ukimchunguza bila mwenyewe kujua. “Mke/mume wangu hajali mambo haya” Hujali kumbe unamteka mwisho wa yote utamnasa.
MPE MAJUKUMU
Ukisha mchagua umpendaye, huwezi kutambua uwezo wake mpaka umpe majukumu ya kufanya. Kwa mfano mtume akalipie maji, umeme au mwagize asimamie jambo fulani.
Ukishafanya hivyo kaa kando mwangalie, anavyoiba chenji, anavyopunguza gharama bila kukushirikisha, lakini baadaye muulize, utashangaa alivyotibua mambo akidhani wewe si mtu wa kujali sana, kumbe ulikuwa umemtega na hatimaye umemnasa.
MUWEKE KWENYE WAKATI MGUMU
Njia nyingine ya kumnasa anayekufichia makucha ni kumweka katika wakati mgumu. Wanasema rafiki wa kweli hujulikana kwa dhiki. Tengeneza dhiki kwa makusudi na kuzitekeleza. Akikuambia naomba unitumie vocha mpenzi au ninunulie nguo mwambie sina pesa, halafu uone kama atakuwa na kiwango kile kile cha mapenzi. Wapo wanaume wengine wa pesa na mishahara ya wapenzi wao, ili kuwabaini ni kuwanyima wakati mwingine.
TUMIA WATU
Katika hali ya kawaida, majirani na marafiki wanawatambua zaidi wapenzi wetu kuliko jinsi tunavyowatambua sisi. Inawezekana kabisa mpenzi wako akawa mtakatifu unapokuwepo lakini ukiondoka anajiachia ile mbaya, hivyo ili kujua tabia zake waulize rafiki na jirani zako watakusaidia kumtabua mpenzi wako.
ANGALIA ANAVYOWATENDEA WENGINE
Wapenzi wengi wanapokuwa wamepata wapenzi hutazama wanavyotendewa wao na kudhani inatosha. Mtu muungwana huwatendea wengine mema. “Aa, mama naye kanichosha kila siku anataka pesa.”
Hebu sikia kauli hii, kama mtu analalamika kuchoshwa na mama yake itakuwaje kwako? Amka na kutambua kuwa anakufichia makucha na ipo siku atakubadilikia hata wewe na kukutesa. Amka usikubali kudanganywa na mpenzi mnafiki.
Saturday, July 27, 2013
Choo Cha Gold Kilicho Nunuliwa Na Kanye West Na Kim Kardashian
Wednesday, July 24, 2013
FIVE SIMPOLE RULES TO BE HAPPY....TARATIBU TANO ZA KUKU FANYA UWE MWENYE FURAHA.
2.free your mind from worries
3.live simply
4.give more
5.demand less expect miracles in life
no one can go back and make a brand new stat
anyone can start from now and make a brand new start endings....
god didn't promise day without pain laughter without sorrow sun without rain but he did promise strength for the day comfort for the tears and light for the ways
disappointments are like road bumps the slow you down but you enjoy the smooth road after wards don't stay on the bumps too long move on.
when you feel down because you didn't get what you want just sit tight and be happy because god has thought of something better to give you
when something happens to you good or bad consider what it means.
there's purpose to life's events, to teach you how to laugh more or not to cry too hard
you cant make someone love you all you can do is be someone who can be loved the rest is up to the person to realize your worth
is better to lose your pride to the one you love than lose the one you love because of pride
we spend too much time looking for the right person to love when or finding fault with those we already love when instead we should be perfecting the love we give
never abandon an old friend you will never find one who can take his place friendship is like wine it gets better us it grows older. when you have something in this five roles you can share what your friends on other social networks.
Jitambue.....SABABU MBOVU ZA KUINGIA KATIKA MAHUSIANO/NDOA (Fahamu kwanini wengi hujuta baada ta muda mfupi)
Wanandoa wengi hawajui nini wafanye, nini waelewe ili kufanya ndoa yao zifanikiwe. Thamani ya ndoa na jinsi ndoa inavyochukuliwa sikuhizi ni tofauti sana na nyakati za wazazi wetu, na hii imewafanya wengine kujikuta wako wenye ndoa kwasababu mbovu na hivyo ndoa nyingi kuvunjika au kuyumba baada ya muda mfupi tu. Vitu kama kudhamiria, heshima na uaminifu sio vya maana tena siku hizi, sababu watu wanaogopa kuonekana wazamani na washamba.
Mtazamo wa ulimengu juu ya ndoa umeharibiwa na magazeti, luninga na vitabu mbali mbali. Siku hizi kuishi bila ndoa ni kitu cha kawaida, kuwa na mpenzi nje ya ndoa sio kitu cha ajabu tena, mapenzi nje ya ndoa sio ya kushangaza hata kidogo. Kinyume chake ukionekana kuyashangaa haya, jamii itakushangaa wewe kwa jinsi ulivyo nyuma ya wakati. Mambo yamebadilika sana, zamani binti akikutwa bikira wakati anaolewa ilikuwa sifa kwake na familia nzima, siku hizi binti akikutwa bikira atachekwa, na watu kumshangaa wakihisi ana matatizo fulani. Hali kadhalika kwa kijana wa kiume aliyejitunza. Kwa bahati mbaya sana tunaishi katika jamii ya ajabu isiyoamini katika kujitoa kwa kweli na kudhamiria katika mahusiano. Jamii isiyoamini katika uaminifu, na ndiyo maana magomvi mengi hutokea pale simu ya mmoja inapoguswa. Kuwindana na kuchunguzana kumekuwa kawaida, maadili sio jambo la kuzingatiwa tena. Wanandoa wengi ni wale wenye majeraha ya moyoni na walio umizwa, kwa hiyo hutoka nje ya ndoa zao wakitafuta mwingine aliyeumizwa kama wao ili waliwazane.
1. Hofu ya umri kupita na kuzeeka
Wako wengi sana, hususani watu wa wajinsia ya kike ambao wamejikuta wakiwakubali wanaume wa aina yoyote ili mradi tu nao waolewe maana umri wao ulionekana kusonga sana na hofu ya kutoolewa kutanda. Mwanaume anayehusiana na mwanamke mwenye tabia hii huulizwa au kulazimishwa kila siku kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa binti au kutangaza ndoa. Ndoa nyingi za aina hii zimeishia kenye talaka na kutengana.
Wako wengine ambao kwasababu wanakiu sana ya kupata watoto na wameogopeshwa sana habari kwamba wana weza wasipate watoto kwa sababu ya umri wao, basi watacheka na kaka yeyote yule ilimradi tu waolewe au wazae naye. Wengine wajinsi hii wamejuta sana baada ya kujikuta kuwa waliyezaa naye hakuwa BABA bali mwanaume tu, tena kirukanjia tu na kwahiyo wanawake hawa wameishia kulea mtoto au watoto wao wenyewe pasipo mzazi wa pili (single parenting), jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linawaathiri watoto wengi. Kwa wale wanaokimbilia kuolewa ili wakazae watoto, kukumbuka kuwa hata huko kwenye ndoa kuna waliokosa watoto.
2. Kuingia katika ndoa/mahusiano kwa lengo la kusaidiwa au kuongeza kiwango cha kiuchumi ulicho nacho.
Hapa wengine wamewageuza wapenzi wao kuwa mitaji au rasilimali ya kuwaondoa wao pamoja na ndugu zao kutoka kwenye umasikini. Kwa kuthibitisha hili wengine wamepewa majina kama BUZI, ATM n.k.
Katika penzi la namna hii hakuna mguso au muunganiko wa kuhisia (intimacy) baina ya wapenzi, bali kinachowaunganisha pekee ni kile kilicho mfukoni au vile vinavyoshikika na kuonekana tu. Athari za penzi la aina hii lina fungua milango mingi kwa wahusika kutokuwa waaminifu na hata kujihusisha na mapenzi nje ya mahusiano yao.
3. Kuingia kwenye ndoa sababu ya mimba au mtoto aliyepatikana kabla ndoa
Lazima kutofautisha kuwa sababu iliyowapelekea kuzaa mtoto siyo itakayowapelekea kuoana. Acha sababu ya kuoana kwenu iwe penzi lenu la dhati na sio mimba au mtoto. Suala hili linahitaji pia wazazi wajue kwamba kitendo cha watoto kupeana mimba au kupata mtoto hakitoshi kuwa sababu ya kuwalazimisha kuoana, maranyingi wazazi wamewalazimisha watoto wao kuingia katika ndoa sababu ya mimba au mtoto na kujikuta wanawaharibia maisha yao mazima. Yanini kujiingiza katika mahusiano yakudumu kisa umempa au umepewa mimba na kuifanya hiyo ndio sababu ya kulazimisha muishi pamoja kama mume na mke wakati kabla ya mimba hiyo hakuna mmoja kati yenu aliyewahi kuwaza kuwa siku mmoja mtakuwa mume na mke, badala yake baada ya kipindi kifupi mnagundua kuwa hakuna penzi baina yenu bali kinacho waunganisha ni mtoto pekee. Maumivu na vikwazo baina yenu vinawadhihirishia wazi kuwa ninyi wawili hamkutakiwa kuwa pamoja bali mmelazimisha tu. Kinacho fuatia hapo ni kufungulia mlango penzi lingine nje au kufanya mkakati wa kusitisha mahusiano yenu ili kuitafuta furaha ya kweli sehemu nyingine.
4. Kulazimika kuingia kwenye ndoa au mahusiano ya kudumu kwasababu ya upweke, (Loneliness).
Mara nyingi mtu anapokuwa peke yake (single) huwaza kuwa ndoa ndiyo inayoweza kuwa utatuzi mkubwa wa matatizo yake. Nakubaliana na ukweli wa maandiko kwamba “Sio vema mtu awe peke yake…” lakini ni vizuri tukijua tofauti iliyopo baina ya kuwa peke yako na upweke. Hivi ni vitu viwili tofauti: kuwa peke yako inamaanisha kukosa mawasiliano au ukaribu na watu wengine, unakuwa kama uliyetengwa (being alone), wakati upweke (loneliness) inahusisha nafsi, akili na hisia (soul, mental and emotions) kuwa pweke au kujihisi kutengwa na hii ni ngumu kuishuhulikia. Ni heri kuwa peke yako (single) kuliko kuwa kwenye ndoa na bado ukajisikia upweke (lonely). Wako wengine waliodhani ndoa ni suluhisho la upweke waliokuwa nao na mara walipoolewa au kuoa, mawasiliano baina yao yakayumba na hivyo kukomaza upweke kwa wote wawili (Not alone but lonely).
5. Kuolewa au kuoa kwasababu ya shinikizo kutoka kwa wazazi, ndugu au marafiki
Shinikizo hizi zaweza kuwa za kihisia au hata kihalisia. Kihisia ni pale ndugu au wazazi wanapokushawishi mara kwa mara kuoa sababu umri wako unaonekana kwenda na wako wazazi wengine husisitiza kuwa wanataka wajukuu (utasikia mzazi anasema unataka nife sijawaona wajukuu zangu?). Hata kama huhisi kulazimishwa lakini kwa kule kurudia rudia kwa kukumbushwa kila siku kunaweka shinikizo ndani yako, kunaathiri hisia zako na kuweza kukupelekea kuingia katika ndoa isiyopangiliwa. Shinikizo la kimwili au kihalisia ni pale wazazi wanopolazimisha watoto wao kuoa au kuolewa na watu fulani kwa sababu tu ni marafiki zao (family friends) au kwa sababu ya kulinda utajiri na matarajio yoyote binafsi. Ndoa nyingi za aina hii zimekuwa kero na dimbwi la maumivu na machozi, baada ya muda kidogo mna jikuta mali mnazo, wazazi wenu wanapatana na kupendana, lakini nyie kama wapenzi ni maadui wakubwa. Jiulizeni mnaingia kwenye mahusiano kwa furaha yenu au ya wazazi wenu?
6. Kuamua kuoa au kuolewa ili kupata uhuru.
Hii hutokea sana kwa wale waliozoea kubanwa sana na wazazi katika kila wafanyacho hususani katika maamuzi. Wengine huzikimbia familia zao maana hazieleweki, hazina mpangilio na hivyo kutamani kutoka ili wakaanzishe zakwao wenyewe. Kinadada na kinakaka wanachoka kuamuliwa na kuwekewa masharti ya kuvaa, kula, kufanya mambo, kutoka na kurudi kwa muda kwahiyo wanadhani ndoa ndio itawachomoa kifungoni hapo. Ninaushahidi wakutosha wa baadhi ya ambao walikimbilia katika mahusiano ili kuwa huru na kwa bahati mbaya waliyoyakuta huko kwenye mahusiano yaliwafanya watamani hali waliyoiacha nyumbani kwao ingawa kwa bahati mbaya wakati huo ‘it was too late’.
Monday, July 22, 2013
FAHAMU JINSI YA KUISHI NA WATU WENYE TABIA YA KULAUMU
- Kama wote mtafuka moto na kuwajeuri au klujibizana hakuna kitakachofanyika, hali itakuwa ngumu zaidi na mlaumu au mlalamishi atapata kitu kingine cha kulaumu juu yako, yamkini akasema wewe huambiliki.
- Kwa vyovyote lawama zitakavyokuwa, fahamu tu kuwa mteja (ikiwa ni kwenye biashara) wakati wote ana haki, fahamu hakuna biashara bila huyo mteja. Hata kama amekosa, mlaumu wakati wote hujiona ana haki ya kutoa malalamiko yake na kusikilizwa. Kwa kunyamaza na kumsikiliza, unatunza kazi yako na kuiendeleza.
- Kama kelele hazitapungua, lawama zaweza kuvuka mpaka na kuwa lawama au shutuma binafsi nahii yaweza kuleta ugomvi binafsi.
- Kwa sababu ni rahisi sana kupandishwa hasira zaidi ya kupooza hasira, ikiwa utamruhusu mlaumu akupandishe hasira, utalazimika kuzielekezea hata kwa watu wengine wasio husika, ambao unahitaji kuwapa huduma pia. Hii sio haki na inawapa mlango mwingine wa kuanza kukulaumu.
- Ukiruhusu mtu akupandishe hasira, kiwango chako cha msongo wa mawazo kitapanda, na hivyo waweza kujikuta unapata matatizo kiafya. Mfano. Kuumwa kichwa mara kwa mara, mgongo kuuma, mshtuko wa tumbo, na mapigo ya moyo kuzidi kasi. BP, wale wenye vidonda vya tumbo huzidi kuuma nk.
- Kuruhusu kupandiswa hasira mara kwa mara kazini, huwafanya wengi kwenda kuzishushia nyumbani, nah ii huleta mfarakano na watu wa kwenye familia. Hasira na migongano hii ikizidi nyumbani, kasi utalala na kuamka nayo na hivyo kwenda nayo kazini asubuhi, hii ukufanya kuanza siku na hasira na hivyo kukuaruzana na yeyote yule.
- Unajua kabisa kuwa, sio jukumu lako kukasirikia kazini dhidiya mteja au wale unaowahudumia, hali hii ikitokea, utajihisi vibaya moyoni, na waweza wapoteza hata wale ulionao karibu na walio marafiki.
NINI TUFANYE KWA MTU MWENYE TABIA YA LAWAMAJitahidi kujiweka huru, mpole na asiyepaniki kwa vyovyote iwezekanavyo (be relaxed as possible) vuta pumzi ndefu, acha mabega na shingo yako iwe huru mbali na hasira na jaribu kuhisi utulivu.Tulia hadi joto na moto wa mlaumu ushuke, ukijaribu kuweka neno hapa, atatulia na kukuamkia tena. Mwili wako uonyeshe mawasiliano, weka pozi la utulivu sio la shari, muangalie machoni, usimkwepe, kama ni kwenye meza, egemea kidogo upande wake kama vile uko tayari kumsikiliza kwa upole.Msikilize anachosema sawia, ikiwezekana chukua karatasi na kalamu akuone ukiandika pointi za kile anachalaumu. Hii itakusaidia kumwonyesha kuwa unamaanisha na hivyo kushuhulikia kile anacholaumu. Pia itakukumbusha wewe nini haswa kilikuwa kinalaumiwa mara baada ya yeye kunyamaza.Baada ya kusikiliza anachokisema, mwonyeshe mlaumu kuwa unahisi sawa na vile anavyojisikia, na hata ingekuwa niwewe ungeumia au ungelaumu pia. Mfano; Mwambie “Naelewa kabisa jinsi ilivyokuudhi hasa kwa jinsi ilivyotokea” hii inamwonyesha anayelaumu kuwa unamuhurumia na kwamba huoni kuwa analaumu tu bila sababu.Pata muda wa kuliangalia tatizo kiundani, sio mara zote mlaumu ana haki, ingawa hauhitaji kumwambia hivyo usoni kwake. Kama ni jambo litakalohitaji muda basi mwombe muda wa kulishuhulikia na muahidi kumpa taarifa baadaye na kweli ufanye hivyo ulivyoahidi.Pale unapogundua kuwa unamakosa katika lile lililokuwa lina laumiwa, basi kuwa mrahisi kuomba radhi na uwe mkweli usitake kufunika mambo na kujitetea.Kamwe usijitetee, hatakama sio wewe mhusika mfano; “Sio kosa langu” mimi sikuwepo jana” kamwone bosi basi “Usilaumu kabla ya kuuliza kwanza” nk. Mlaumu hana muda wa kujua nani ni mhusika ili amlaumu yeye. Ukitupia lawama kwa wengine kama ni kwenye ofisi au kampuni basi unafanya wateja au mteja kupoteza imani na ofisi au wafanyakazi wengine.Kinachotakiwa, fanya kile uwezacho kupunguza tatizo, na mlaumu akuone ukiwabize kulifanya hilo. Mara utakapo mweleza kuwa unafanya kitu basi akuone ukikifanya muda huo.Usishangae, hata mtu unaemjua kuwa ni mpole, anaweza kuwa mkali mara tu anapogeuka kuanza kuwa mtoalawama, na hasa kama sio mara ya kwanza kwa tatizo la jinsi hiyo kutokea. Ni ngumu kuanza tu kushuhulikia kila anachokilaumu kabla kwanza hauja shuhulikia hisia zake. Sungumza nae kwanza. Mruhusu amalize kuongea ili apoe. Tingisha kichwa taratibu kuonyesha uko na yeye, akimaliza ongea taratibu.
Lawama kwa njia ya simu:Katika hali hii, yakupasa ujitahidi kuwa mpole, hata kama hiyo simu inaingilia mambo na ratibu zako za kazi, najua hii ni ngumu hasa ukizingatia kuwa mlaumu hakuachii hata nafasi ya kumsikiliza, bali anafuka tu kama moto.Weka kalamu na karatasi karibu na wewe mara zote (kama ni ofisini) akiacha nafasi kidogo, muulize jina lake na ikibidi anapiga simu kutoka wapi, au ofisi gani, kama huna uhakika mwambie akutajie tarakimu za jina lake au la ofisi.Kama kuna kitu utalazimika kuangalia katika mafaili, vitabu au computer, basi muulize kama angependelea kusubiria katika simu (hold on) au angependa kukata simu na umpigie baada ya muda kidogo.
Kamwe usiweke mkono katika kisemeo (ikiwa ni simu ya mezani) mlaumu atajua kwamba umeamua kumfanyia ukatili na hutaki kumsikiliza. Hii ni kwa sababu simu za sasa zimetengenezwa katika hali ambayo sauti inapita sawa katika sehemu ya kuzungumza na sehemu ya kusikilizia.Ikiwa unataka kumkatisha mlaumu, wakati wote. Jaribu kumwita kwa jina lake, hii itamfanya atulie kukusikiliza zaidi ya kusema “samahani” “unajua”, ni kweli…..”Kama ni kitu ambacho hautaweza kukishuhulikia muda huo, muahidi kukishuhulikia baada ya muda fulani na ujitahidi kuwa mwaminifu katika ahadi yako na atarajie majibu ya kutia moyo. Mpe jina lako, pia, ili ajue ninani wa kuwasiliana nae ikiwa atahitaji kupiga simu tena. Hii itamjengea imani ya kuwa, unamaanisha kumsaidia. Hata kama bado mambo hayajamalizika basi umpigie katika muda ulioahidi ili kumpa ripoti ya kunachoendelea. Kama hautaweza kulishuhulikia wewe, basi muahidi kumpa mtu muafaka wa kumsaidia, nawewe uwe karibu kuhakikisha madai yake yanashuhulikiwa.
Labda kosa laweza kuwa lako, ikiwa hivi, basi kubali na kumtaka radhi, jaribu kumwelezea jinsi utakavyojitahidi kuweka mambo sawa, kamwe usijitetee wala kutupia lawama kwa wengine. Hali hii itakufanya uonekane dhaifu na mkwepa majukumu. Unapokubali na kushuka mara nyingi mlaumu nae huwa muelewa.Ikiwa unaona lawama zinakuwa kubwa na kushindwa kuzitafutia ufumbuzi haraka basi tafuta eneo au upenyo wa maafikiano, hii itafanya kasi ya ujeuri wa mlaumu kupungua kwasababu ni ngumu yeye kuendelea kupigizana kelele na mtu anae afiki kila usemalo.
Lawama hizi za njia ya simu huwa zaidi katika ulimwengu wa biashara, lawama hizi huleta matatizo mengi zaidi.
Watu wengine ambao hawawezi kulaumu uso kwa uso, huwa rahisi kwa kutupa lawama kupitia simu. Katika biashara, au maofisini, hali huwa ngumu zaidi maana, unakuta mlaumu kashapiga simu kwa secretari (katibu muhtasi) nayeye akamruhusu mtu huyo aongee nawewe, basi anakuja na hasira mara dufu. Kama secretari sio mchapakazi na labda amechelewa kumuunganisha mlaumu huyu na wewe basi mlaumu anaweza kutakamani kukupasukia mara anapokupata wewe kwenye simu. Watu wengi huchemka zaidi kwenye simu zaidi ya wanavyokuwa ana kwa ana, hali hii hufanya maelewano kuwa magumu zaidi.
Kwa sababu hauwezi kuona sura ya huyo anayelaumu, wala mwili wake ni vigumu mmoja wenu kupoa maana haujui jinsi anavyojielezea au jinsi gani anamaanisha kutafuta suluhu.
KUNDI LA SCOPION GIRLZ KWISHA HABARI YAKE,SASA VIPANDE VIPANDE..WATUPIANA NGUO NJE
MEMBA wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wametofautiana hadi kufi kia hatua ya kutukanana na kutupiana nguo nje.
Mpango mzima ulitokea hivi karibuni Kijitonyama jijini Dar, nyumbani kwa Isabela ambapo chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Isabela kumsifi a mtandaoni X-memba wa kundi lao, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ kwa kununua gari, ndipo Kabula alipokasirika na kuanza kumtukana Bela na mama yake matusi ya nguoni.
“Sikumuelewa kabisa Jini, kumsifi a Jack kuhusu kumiliki gari ndiyo kumemfanya anitukane? Iliniuma sana na sitamsamehe, bora kila mtu achukue hamsini zake, nguo zake nilimtupia nje,” alisema Bela na kusisitiza kufanya muziki peke yake kwa sasa
Friday, July 19, 2013
MAJAMBAZI WATEKA KITUO CHA POLISI
Hii imetokea huko Gongolamboto jana ,majambazi waliokuwa wamejihami kwa
silaha za kisasa walivamia kituo Kidogo cha polisi kilichoko
Gongolamboto na kuwateka polisi waliokuwemo kituoni humo na kuwafungia
mahabusu ya kituo hicho, majambazi hao pia waliwajeruhi na walitaka
silaha zaidi na radio call, hata hivyo walishindwa kwakuwa radiocall
haikuwa na chaji(aibu nyingine ya jeshi la polisi) waliondoka wakiwaacha
polisi ndani ya lockup yao mpaka walipokuja kuokolewa na wananchi
Source; Radio Wapo, Radio Tumaini
Source; Radio Wapo, Radio Tumaini
Wednesday, July 17, 2013
NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE COMPUTER YAKO.
Wengi wanalalama kuwa cm zao hazina whatsapp au wanashanga vipi mie napatikana kwenye hiyo mambo wakati na cm yangu ni ya Tochi tu.
Hebu cheki maelekezo hapo chini ukimaliza kumbuka kuni Add na mimi ili tutumiane ma picha na mambo mengine….
Download App inaitwa Bluestack Kutoka hapa Run Mobile Apps on Windows PC or Mac with BlueStacks | Android App Player then Run Hyo app so Utakua na Access na Playstore so utaweza Kudownload App zote Ikiwemo Whatsapp Instagram, viber, tango, na nyingineee tu.
ila Hyo App Ni ina Mb 8 tu ila inahtaji Specs kubwaaa kwanza Ram Lazma Iwe 2gb Pia Graphic accelerator lazma ziwe Updated… So Kabla Ya Kudownload Na Kuinstall Fix Hzo kwanzaaa
Ukisha insall bluestack, ingia kwenye google play install go launcher ex, itaifanya hiyo bluestack iwe na mwonekano mzur wa android kama za cm, bt kunakua hakuna mwingiliano wwte kati ya pc na bluestack mfano ukitaka kutuma picha kwa kutumia watsapp na kama hiyo picha imo kwenye pc, inatakiwa ui install dropbox kwenye pc yako.
Kumbuka, youwave ni yakulipia (Ingawa unaweza kuichakachuwa) ila bluestack ni ya bure, isipokuwa ina ishu za ram, vga drivers etc.
NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE COMPUTER
Wengi wanalalama kuwa cm zao hazina whatsapp au wanashanga vipi mie napatikana kwenye hiyo mambo wakati na cm yangu ni ya Tochi tu.
Hebu cheki maelekezo hapo chini ukimaliza kumbuka kuni Add na mimi ili tutumiane ma picha na mambo mengine….
Download App inaitwa Bluestack Kutoka hapa Run Mobile Apps on Windows PC or Mac with BlueStacks | Android App Player then Run Hyo app so Utakua na Access na Playstore so utaweza Kudownload App zote Ikiwemo Whatsapp Instagram, viber, tango, na nyingineee tu.
ila Hyo App Ni ina Mb 8 tu ila inahtaji Specs kubwaaa kwanza Ram Lazma Iwe 2gb Pia Graphic accelerator lazma ziwe Updated… So Kabla Ya Kudownload Na Kuinstall Fix Hzo kwanzaaa
Ukisha insall bluestack, ingia kwenye google play install go launcher ex, itaifanya hiyo bluestack iwe na mwonekano mzur wa android kama za cm, bt kunakua hakuna mwingiliano wwte kati ya pc na bluestack mfano ukitaka kutuma picha kwa kutumia watsapp na kama hiyo picha imo kwenye pc, inatakiwa ui install dropbox kwenye pc yako.
Kumbuka, youwave ni yakulipia (Ingawa unaweza kuichakachuwa) ila bluestack ni ya bure, isipokuwa ina ishu za ram, vga drivers etc.
Subscribe to:
Posts (Atom)